Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge ‘#BongoIce’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula.
Hii ni kutokana na kampeni inayoendelea mitandaoni iitwayo #ALSIceBucketChallenge ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.
Mkurugenzi wa Vodacom, Rene...