Kikao cha Halmashauri Kuu kimeendelea sasa hivi kwa zaidi ya saa nne hapa Makao Makuu ya CCM Dodoma, viko vitu vingi vinaendelea nje ya Ukumbi… wapo wanaoimba na kushangilia, wengine wapo wakiendelea kusubiri kile kitakachotangazwa baada ya Halmashauri Kuu kumaliza Kikao.
Watu ni wengi sana nje ya Ukumbi, nimebahatika kukutana na wenyeji wa Mji wa Dodoma na watu ambao wanafanya shughuli zao kwenye Majengo yanayozunguka Makao Makuu hayo,...