Wednesday, August 27, 2014

UMESHASIKIA KUHUSU ALS ICE BUCKET CHALLENGE? SASA VODACOM WAMEKUJA NA HII KWA WABONGO..!!

Screen Shot 2014-08-27 at 7.36.01 AMKampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge ‘#BongoIce’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula.
Hii ni kutokana na kampeni inayoendelea mitandaoni iitwayo #ALSIceBucketChallenge  ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.
Mkurugenzi wa Vodacom, Rene Meza amekuwa wa kwanza kushiriki kampeni hii na kuwateua Naibu Waziri wa Mawasiliano January Makamba, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel ndugu Sunil Colaso kushiriki kampeni hii.
Tazama ilivyokuwa hapa chini..

Thursday, August 21, 2014

A WORD OF THANX..

And finally, we reached those six digits.. 101,012+ Viewers. As this page grows day by day, i would like to take this opportunity to thank all of you who support this blog.Our blog site is gaining popularity because of you, our beloved visitors.. We will always try our best to keep you guys updated, so please keep visiting..
Sincerely,
ALOYCE JERRY,
Founder of Aljerry'12




Special Thanx to all the supporters and viewers, here is to mention the few:





Tuesday, August 19, 2014

BRAND NEW: KUTOKA KWA CHID BENZ CHUMA, HII NDIYO TRACK YAKE MPYA AKIWASHIRIKISHA DIAMOND NA AY..

Baada ya kimya cha muda mrefu,, Dully sykes sasa amrudisha tena Chid Benz kwenye Game. Hii ndio track mpya toka kwake akimshirikisha rais wa wasafi, Diamond Platnumz na Mr. Cash money himself, Ambwene Yesaya 'AY'.. sikiliza na download pini hiyo kali hapa...

Kutoka kwa Machalii ya Ara.. Hii ndio Remix ya Mamong'oo Toka kwa Jambo Squad ft Arusha United


Katika remix hii kali, utasikia vichwa vikali toka pande za kaskazini, Arusha City, kama vile Stoppa Rhymes, Nick wa Pili, G.Nako, Bu-Nako, Chindo, Ruff-G, Nakaaya, Chief Mufasa na Wengine wengi..
Download na sikiliza pini hii kali hapa..


Friday, August 15, 2014

BRAND NEW: KWA WALE WAPENZI WA MUZIKI WA MJ,, HII NDIYO VIDEO MPYA TOKA KWA MAREHEM MICHAEL JACKSON

mj
Michael Jackson angetimiza miaka 55 mwezi huu lakini bado mashabiki wa muziki wake wanaendelea ku-enjoy kazi zake kama hivi. Kuelekea kutoa album ya Xscape ya Michael Jackson, hivi sasa imetoka video mpya ya A Place With No Name.
Video hiyo zaidi ya kuwa na wahusika wengine, pia imehusisha baadhi ya video za Michael Jackson kutoka kwenye behind the scene wakati aki-shoot short film ya In the Closet.

HIZI NDIO KAULI TATA ALIZOANDIKA DIAMOND KWENYE UKURASA WAKE WA INSTAGRAM..!!!

dd
Story ya kwanza ni kuhusu ujumbe mrefu aliondika Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram. Ujumbe huo unaonekana unaenda kwa msanii fulani japokuwa hakuweka wazi ni msanii gani. Diamond aliweka post hii na baada ya muda mfupi aliifuta lakini maneno yote yalikuwa yanasomeka hivi.
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!
Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike”.

HILI NDIO TAMKO LA WIZARA YA AFYA KUHUSIANA NA EBOLA KUINGIA TANZANIA..

Screen Shot 2014-08-15 at 10.47.21 AMUgonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
Screen Shot 2014-08-15 at 10.47.06 AMWaziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza.

Sunday, August 3, 2014

Hizi ni baadhi ya picha ya vipande vikali katika Video mpya ya Niki wa Pili, Sitaki kazi, itakayokujia hivi karibuni!

0
Picha zote ni kutoka kwenye instagram ya Nikk wa Pili zikiwa ni kati ya sehemu ya uchukuaji wa video ya Sitaki kazi. Wimbo huo ameufanya pamoja na Ben Pol & G Nako
1
2
3
4

Friday, August 1, 2014

VIDEO: TAZAMA KALI HII,, KIKWETE AKIWA SOKONI NA MAMA SALMA WAKINUNUA SAMAKI..



Hii ndio video iliyowashangaza watu wengi ikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa sokoni na mama Salma wakiwa wananunua samaki.. Hii inafurahisha kwa kweli. Tazama video yenyewe hapa chini..

Wednesday, July 30, 2014

Hii ndio ajali mbaya iliyotokea Dodoma leo asubuhi..!!!

Capture5July 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.
Capture4Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Capture3Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.
Taarifa ya kamanda wa Polisi inseam katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5. Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga busi hilo.

Saturday, July 26, 2014

BRAND NEW: Barnaba na Mkewe katika video yake hii mpya,, Icheki Hapa..!!!

Screen Shot 2014-07-26 at 2.30.12 AMHii single inaitwa ‘Wahaladee’ ambayo ni miezi kadhaa imepita tangu utoke rasmi kwenye Radio lakini July 25 2014 Watanzania wameletewa video yake ambayo imeongozwa na Nick Dizzle ambapo kingine kikubwa kwenye hii video ni mrembo alieigiza ndani yake, ni mke wa ndoa wa Barnaba (Mama Steven)
Naambiwa video imefanywa Kenya na Tanzania.

Thursday, July 24, 2014

Hiki ndicho kilichoendelea Mahakamani katika kesi ya Mbasha Jana..!!!

Mbasha 22KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.
Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani.
Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.
Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.
Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Mbasha 25
Mbasha akiwa na baba yake mzazi Mahakamani.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.
Source>>Millard Ayo<<

Tuesday, July 22, 2014

HII NDIO ZAWADI ALIYOITANGAZA DIAMOND KWA MSHINDI WA ZOEZI HILI..!!

ddddsHaya ni maneno ya Diamond akitangaza kitu ambacho ukikifanya unaweza kujishindia milioni moja cash. Soma hapa na kama lipo ndani ya uwezo wako fanya ujishindia pesa kutoka kwa Diamond.
diaondd