Blogger Widgets

Friday, April 26, 2013

MBUNGE WA ARUSHA MJINI AVAMIWA NA POLISI NA KUKAMATWA USIKU WA MANANE NYUMBANI KWAKE!!!

Godbless Lema alipowasili chuo cha Uhasibu Arusha  Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, ametiwa hatiani na jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi wa vurugu zilizojitokeza siku ya jumatano katika chuo cha uhasibu Arusha. Pia imedaiwa kuwa mbunge huyo ndiye aliyesababisha wanafunzi wa chuo hicho wamfanyie vurugu mkuu wa mkoa wa Arusha alipofika katika eneo hilo. Usiku wa kuamkia Leo, Polisi wamevamia nyumba ya Mbunge...

Wednesday, April 24, 2013

Habari kamili na picha juu ya tukio la mgomo wa Wanafunzi Chuo cha Uhasibu Arusha..

Reported by Aloyce Jerry Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka...

MABOMU YA MACHOZI NA RISASI ZATUMIKA KUWATULIZA WANAFUNZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA!!!!

Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha chalazimika kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wametanda chuoni hapo na kugoma kumsikiliza mkuu wa mkoa, kwa madai kwamba ana dharau. Mabomu na risasi zilirindima eneo hilo huku wanafunzi wakikimbia hovyo huku na kule kwa hofu na woga. Picha na habari zaidi zitakujia hapa hapa......

MKUU WA MKOA AGOMA KUONGEA NA WANAFUNZI KWA MADAI HAWEZI KUONGEA BILA KIPAZA SAUTI!!!

Baada ya mkuu wa mkoa kufika chuo cha uhasibu Arusha, alishindwa kuongea na wanafunzi hao kwa madai kwamba hawez kuzungumza bila kipaza sauti. "Mkuu wa mkoa mwenyewe anaitwa hapa kwenye tukio anakuja kama anakuja kwenye send-off wakati kaitiwa msiba hapa" Ni maneno ya mbunge wa jimbo la Arusha bwana Godbless Lema.. pia Lema amesikika akisema "Mkuu huyo wa mkoa amekuja hapa si kwa ridhaa yake, bali ni cheo tu kimemleta hapa" Wanafunzi wa chuo hicho...

BREAKING NEWS!!!!! YANAYOJIRI NOW CHUO CHA UHASIBU ARUSHA!!!

Wanafunzi wagomea masomo na kudhamiria kuandamana kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kisu usiku wa jana, saa nne usiku wakati akitokea chuo kujisomea. Katika picha ni matukio yanayoendelea sasa chuoni hapo, wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha bwana Godbless Lema..  KINACHOENDELEA NOW KATIKA PICHA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA... ...