Blogger Widgets

NEWS

Hivi ndivyo Majambazi walivyofanya Mauaji Arusha jana
Screen Shot 2014-06-02 at 8.32.39 AMKutoka Arusha, tumepata ripoti kwa ufupi kwamba majambazi waliingia kwenye
 duka moja la kubadilishia fedha Clock tower karibu na house of wine Arusha mjini ambapo 
kifo cha huyu ndugu kilitokana na yeye kupiga kelele baada ya kuona majambazi hao 
wakitenda uhalifu.
Taarifa za mwanzo zinasema Marehemu alipiga kelele hizo muda mfupi tu baada ya 
kutoka kanisani na akawa anasubiri watoto wake kwenye eneo la tukio ila alipoona 
dada ndani ya duka kavamiwa ndio akaanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Screen Shot 2014-06-02 at 8.33.35 AM

Rais masikini zaidi duniani. Unamfahamu?


Rais Jose Mujica akiwa na Papa Francis
Sifa kwa wanasiasa kokote duniani ni nadra, hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu wamemmiminia sifa Rais wa Uruguay baadhi wakitamani kama marais wao wangekuwa kama Rais Jose Mujica wa Uruguay.
Kwenye Twitter kuna zaidi ya ujumbe laki moja wa watu nchini Uhispania wakitamani kama waziri mkuu wao angekuwa kama Rais Maskini zaidi duniani Jose Mujica wa Uruguay.
Rais huyo anasifika kwa kuendesha gari kuu kuu , kuishi maisha ya watu wa kawaida na sehemu kubwa ya mshahara wake yeye hupatia mashirika ya misaaada ya kibinadamu...kiasi kwamba anajulikana kama Rais masikini zaidi duniani.

Rais Mujica (Kushoto) na waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy (Kulia)
Na ndio maana waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy huenda asifurahie sana kufananishwa na Rais wa Uruguay.
Lakini swali ni watu wangapi duniani wanaweza kufananisha Rais Uruguay na marais wao? Ni Marais wangapi duniani wanatoa mishahara yao kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu, kuishi maisha ya kawaida na kuendesha gari lililochoka?
Baadhi ya wananchi wanahoji kwa nini nchi kama Uruguay ambayo haina uchumi mkubwa ina huduma bora zaidi kwa jamii kuliko Hispania ambayo imekomaa kiuchumi wakati rais wake hana uchu wa madaraka na tamaa ya pesa?

Mitandao ya kijamii hutumiwa sana kwa mijadala kama hii. Swali ni je nani ana jambo zuri la kusema kumhusu Rais wake hasa katika hizi nchi zetu za Afrika? Unadhani kiongozi yupi barani Afrika anaweza kufananishwa na huyu Rais wa Uruguay? Je kuna Rais asiyeishi maisha ya kifahari enzi hizi?  Source>> BBC Swahili








Wogonjwa wa Dengue kuongezeka!!!
mbu db075
Na Hudugu Ng'amilo
Homa ya dengue inaendelea kushika kasi nchini baada ya takwimu za Januari hadi juzi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuonyesha kuwa watu 376 wamekwishagundulika kuugua ugonjwa huo.
Mtaalamu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa wa wizara hiyo, Dk Janeth Mugamba alisema hadi jana watu wawili walikuwa wamepoteza maisha, idadi ambayo alisema inaweza kuwa kubwa zaidi endapo upimaji utafanyika katika kila wilaya. "Pengine idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kwa sababu wengi hawapimwi, Ijumaa (kesho) tutatoa, taarifa zaidi," alisema.
Alisema Wilaya ya Kinondoni ina wagonjwa wengi zaidi, ikifuatiwa na Ilala na Temeke. Hata hivyo, alisema huenda wilaya zenye idadi ndogo ya wagonjwa hazijaweza kupima na kubaini watu wenye maradhi hayo ikilinganishwa na Kinondoni.
Juzi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema hali ni mbaya na wananchi wanatakiwa kuchukua hadhari wasipate maambukizi ya ugonjwa huo.
Mtafiti wa malaria, tabia za mbu na mazingira, wa Taasisi ya Afya ya Ifakara, Dk Nicholas Govela alisema tayari wameshatuma maombi ya kufanya utafiti wa kina kuwajua mbu wanaoeneza homa ya dengue nchini. "Utafiti huu utasaidia kujua ni mbu kiasi gani wameathirika na virusi hivyo. Tukifanya hivyo tutajua ukubwa wa tatizo, tutajua wanapatikana wapi zaidi na virusi vyao vimetokea wapi," alisema.
Dk Govela alisema ni lazima utafiti huo ufanyike ili kudhibiti maambukizi zaidi ya homa hiyo akisema zipo sababu kadhaa zinazohisiwa kusababisha maradhi hayo, ikiwamo ya wahamiaji kuleta virusi hivyo vinavyosababisha homa hiyo na kuambukizwa kwa njia ya kuumwa na mbu.
"Ugonjwa huu umeenea zaidi nchi za Amerika ya Kusini na Kusini mwa Bara la Asia. Hapa kwetu mbu hawa walikuwapo lakini ugonjwa wa dengue haukuwapo kwa kiasi hiki, ndiyo maana sababu zinazohisiwa zaweza kuwa ni wahamiaji," alisema.
Alisema maambukizi ya homa ya dengue hutokea baada ya mtu mwenye ugonjwa huo kuumwa na mbu hao aina ya Aedes Egyptiae na mbu hao wakichukua virusi, huvisambaza kwa watu wengine. "Inawezekana tatizo ni kubwa zaidi ya hivi inavyofikiriwa kwa sababu wanaokuja hospitali kupimwa na kugundulika ni wachache, wengi wasiofika hawawezi kujulikana," alisema.
Makazi duni hatarini zaidi
Daktari Kiongozi na Mtaalamu wa homa ya dengue, Mrisho Rupinda alisema watu wanaoishi katika makazi duni wapo hatarini kuathiriwa zaidi kwa sababu ya kuwapo kwa taka nyingi na madimbwi.
Alitoa mfano wa wagonjwa wa kwanza wilayani Kinondoni, akisema walitokea maeneo ya Kambangwa, Mwananyamala Komakoma ambako kulikuwa na madimbwi na bwawa la maji.
"Wagonjwa wengi huonekana zaidi kwenye makazi duni kwa sababu ya mpangilio mbovu na kuzagaa kwa taka. Lakini pia maeneo mengine ambayo watu huhifadhi maji kwenye matenki au ndoo kwa muda mrefu bila kuyafunika," alisema.
CHANZO MWANANCHI







Maadhimisho ya Muungano katika picha..


8
12
10
9
7
2
3
4
5
6
1





 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride...

..