TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIRais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete. Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.Tarehe...