Blogger Widgets

Monday, August 19, 2013

HIVI NDIVYO YULE TRAFIK FEKI ALIVYOANZA KAZI!!!


SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari 'feki' wa Usalama Barabarani mwenye cheo cha Sajini, akifanya kazi ya kuongoza magari eneo ya Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam, mambo mapya yamezidi kubainika juu ya sababu za mtu huyo kujiingiza katika kazi hiyo bila kutambuliwa na Jeshi la Polisi.
Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya kuaminika, zinasema trafiki huyo 'feki', ambaye inadaiwa jina lake halisi ni James Juma Hussein (45), mkazi wa Kimara Matangini, alianzia kazi hiyo mkoani Singida kabla ya kujipa uhamisho wa kikazi kwenda Dar es Salaam..