Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu na nabii huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa
Saturday, March 22, 2014
HII HATARI,, NABII GEORDAVIE (NGURUMO YA UPAKO) NA MSAFARA WENYE ULINZI KULIKO HATA RAIS WA NCHI..!!
Wale wa Man UTD, mechi hizi zote Van Persie hatacheza..
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie amepata majeruhi ya goti baada ya kuumia katika mchezo wa raundi ya pili wa hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Olympiakos uliopigwa katika dimba la Old Trafford, jumatano wiki hii.
Van Persie ambaye alifunga hat trick iliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali alitolewa nje na machela katika mchezo huo katika dakika za mwisho, na baada ya kufanyiwa vipimo kiundani imegundulika amepata majeruhi yatakayomuweka nje kwa muda wa wiki 4-6.
Kwa maana hiyo mdachi huyo atazikosa mechi zifuatazo
Mar 23: West Ham (A)
Mar 25: Man City (H)
Mar 29: Aston Villa (H)
Apr 1: Bayern Munich (H)
Apr 5: Newcastle (A)
Apr 9: Bayern Munich (A)
Apr 20: Everton (A)
Apr 26: Norwich (H
Mar 25: Man City (H)
Mar 29: Aston Villa (H)
Apr 1: Bayern Munich (H)
Apr 5: Newcastle (A)
Apr 9: Bayern Munich (A)
Apr 20: Everton (A)
Apr 26: Norwich (H
Friday, March 21, 2014
Ajali mbaya kituo cha mabasi Ubungo..!!!
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la Ubungo, kwenye lango kuu la kuingilia mabasi yatokayo mikoani. Ajali imehusisha magari 6 likiwemo UDA.
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la Ubungo, kwenye lango kuu la kuingilia mabasi yatokayo mikoani. Ajali imehusisha magari 6 likiwemo UDA.
Mpaka sasa haijajulikana idadi ya watu waliopoteza maisha. Hatua za uokoaji zinaendelea.
Taarifa zaidi na picha zitakujia kupitia hapa hapa..
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la Ubungo, kwenye lango kuu la kuingilia mabasi yatokayo mikoani. Ajali imehusisha magari 6 likiwemo UDA.
Mpaka sasa haijajulikana idadi ya watu waliopoteza maisha. Hatua za uokoaji zinaendelea.
Taarifa zaidi na picha zitakujia kupitia hapa hapa..
Wednesday, March 12, 2014
Hiki ndicho alichofanya Christiano Ronaldo baada ya kutajwa kuwa mwanasoka Tajiri ulimwenguni..
Baada ya kutajwa na mtandao wa habari za michezo wa Goal.com kuwa mwanasoka tajiri kuliko wote Ulimwenguni, Cristiano Ronaldo amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpatia sifa ya kuisadia wale wenye matatizo.
Kwa mujibu wa gazeti la kihispania AS ni kwamba Ronaldo ameamua kumlipia fedha za matibabu mtoto mwenye miezi 10 Erik Ortiz Cruz ambaye ni mgonjwa sana akisumbulia na matatizo kwenye ubongo wake (Cortical dysplasia.)
Kutokana na taarifa za kitabibu ugonjwa huu kawaida humfanya mtu awe anapata mshtuko unaoweza kupelekea kuzimia mara 30 kwa siku, hivyo kutokana na hali hiyo mtoto unamfanya mtoto huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa hali hiyo isiyo ya kawaida kwenye ubongo.
Kila kipimo anachofanyiwa mtoto huyo kina gharama ya 6,000 euros na upasuaji mzima unagharimu kiasi cha 60,000 euros hivyo watu wa kijiji cha Villaluenga de la Sagra, Spain, wamekuwa wakijaribu kukusanya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo kupitia michango.
Jambo hili lilipomfikia Ronaldo ambaye alifuata aweze kutoa jezi yake na viatu vyake ili vipigwe mnada, akawapa walichotaka kwa ajili ya mnada na kisha akalipia gharama zote za matibabu ya mtoto huyo.
Kutoka bungeni,, Huyu ndio mwenyekiti wa kudumu wa Bunge la katiba baada ya uchaguzi wa leo..
Hatimae Samuel Sitta ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge la katiba kwa kupata jumla ya kura 487 kati ya kura zote 563 zilizopigwa na wawakilishi wa bunge hilo,na kwa sasa Samuel Sita anatoa hotuba yake ya shukrani kama Mwenyekiti.
Samuel John Sitta amewahi kuwa Spika wa Bunge la tisa na sasa ndiye Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba baada ya kushinda kwa kura 487 dhidi ya 69 alizopata mpinzani wake ambae ni Hashim Rungwe.
Kesho March 13 zitapigwa kura kumtafuta Makamo Mwenyekiti wa Bunge hili ambapo kulingana na sababu za kimuungano atatokea upande wa Tanzania visiwani(Zanzibar) na kuweka usawa wa jinsia kwa hivyo atakaechaguliwa kutoka huko atakuwa ni Mwanamke.
Saturday, March 8, 2014
Subscribe to:
Comments (Atom)



