Blogger Widgets

Saturday, March 22, 2014

HII HATARI,, NABII GEORDAVIE (NGURUMO YA UPAKO) NA MSAFARA WENYE ULINZI KULIKO HATA RAIS WA NCHI..!!

ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake.

Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara hivi karibuni ulishuhudiwa msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea mjini humo.

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu na nabii huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa