Blogger Widgets

Sunday, April 13, 2014

BREAKING NEWS: MLIPUKO UNAOSADIKIWA KUWA WA BOMU WAITIKISA ARUSHA!!



Kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.

Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia vibaya na wamekimbizwa hospitali za Mount Meru na Selian. Kwa sasa Jeshi la polisi limelizunguka eneo hilo kwa uchunguzi zaidi.. Bado hakuna taarifa ya vifo vyovyote vilivyotokana na tukio hilo. Taarifa zaidi tutaendelea kuwajuza..