Blogger Widgets

Wednesday, July 16, 2014

Yanga sasa wameamua, Wasajili mwingine tena toka Brazil

jajaWiki chache baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa kibrazil Andrey Coutinho – klabu ya Yanga leo hii imefanya usajili mwingine wa mchezaji kutoka Brazil.
Usajili wa sasa ni wa Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos Santana “Jaja” ambaye amewasili leo mchana jijini Dar es salaam akitokea jijini Sao Paulo tayari kwa kuanza kazi ya kuitumikia klabu ya Young Africans Sports Club kwa msimu wa 2014/2015.
Jaja ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji wa pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.
Usajili wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha msimu ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.
Jaja anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo Andrey Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.
Kesho asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa ni sehemu ya maandaliz ya michuano mbalimbali itayowakabili.