Taarifa iliyoripotiwa na shirika la utangazaji Uingereza BBC imesema kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram kimefanya mashambulizi katika kijiji cha Adamawa kilichopo Kaskazini Magharibi ya Nigeria na kuteka wanawake na wasichana katika kijiji hicho.
Utekaji wa wasichana na wanawake hao unatokea ndani ya siku sita tangu serikali ya Nigeria na kikundi hicho walipofanya makubaliano ambapo Boko Haram waliahidi kuwaachilia huru zaidi ya wasichana...