Utekaji wa wasichana na wanawake hao unatokea ndani ya siku sita tangu serikali ya Nigeria na kikundi hicho walipofanya makubaliano ambapo Boko Haram waliahidi kuwaachilia huru zaidi ya wasichana 200 wanaoshikiliwa na kikundi hicho.
Japo Boko Haram wamekiuka makubaliano waliyoafikiana Ijumaa iliyopita, bado serikali ya Nigeria ina matumaini ya kuachiliwa huru kwa wasichana hao baada ya kikao kinachotarajiwa kufanyika muda wowote kuanzia sasa huko Chad.