Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarifu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Noorah, Dark Master na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.