Ajali nyingine tena imetokea Tanga leo APRIL 9 2015, taarifa za awali zinasema watu 10 wamefariki na wengine wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni Tanga, gari zilizopata ajali hiyo ni basi la NGORIKA, jingine la RATCO pamoja na gari nyingine ndogo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, RPC Juma Ndaki kathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba mwendo kasi umechangia kutokea ajali hiyo.
Hizi ni PICHAZ ambazo zimeenea mitandaoni zikionesha jinsi hali ilivyo eneo la tukio.