Blogger Widgets

Saturday, April 12, 2014

Mjue msanii wa Bongo aliyepata shavu kushiriki kwenye wimbo maalum wa Kombe la Dunia Brazil..!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith  Wambura ‘Lady JayDee’ kupitia kampuni ya Coca-Cola Tanzania  amepata nafasi ya kushiriki kwenye wimbo maalum kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia itakayofanyika Brazil  mwezi juni mwaka huu.



Katika hiyo ngoma Lady Jay Dee na David Correy wameimba kwa kutumia lugha ya kiingereza huku Octoppizo akiwa amerap kwa lugha ya kiswahili. Wimbo huo ambao umetambulishwa na Kampuni ya Coca Cola wakiwa wanazindua promosheni yao ya Kombe la Dunia itakayowezesha wateja wao kujishindia zawadi mbalimbali.