Blogger Widgets

Tuesday, April 29, 2014

Uliona hii? Cheki jinsi Beki wa Barcelona alivyokula ndizi aliyorushiwa na washabiki kama ishara ya ubaguzi wa rangi..!!

Mchezaji wa Barcelona, Dani Alves, juzi alitoa kali ya mwaka baada ya kula ndizi aliyotupiwa  na washabiki wa timu pinzani kama ishara ya ubaguzi wa rangi.. Tukio lilitokea juzi jumapili katika mchezo baina ya club ya Barcelona na Villareal.


Mchezaji huyo Raia wa Brazil alikuwa tayari kupiga kona mara ghafla ndizi iliyorushwa kutoka kwa washabiki ilitua mbele yake na kwa ujasiri aliokota ndizi hiyo, akaimenya na kuila kisha akapiga kona iliyozaa bao la ushindi kwa wababe hao wa spain...
Chekii video ya tukio hilo hapa...



Katika Mchezo huo Barcelona wallibuka na ushindi wa goli 3 dhidi ya 2 za wapinzani wao villareal.

Vitendo vya ubaguzi wa rangi vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara katika michezo hasa mpira wa miguu. Shabiki aliyebainika kufanya kitendo hicho ni wa Villareal na sasa anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa maisha kuingia katika viwanja vya michezo na kunyang'anywa kadi ya uanachama wa club yake. Club ya Villareal iliomba radhi kutokana na tukio hilo.