Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul "Diamond Platinumz" Usiku wa Jana May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).
Diamond amejinyakulia tuzo zifuatazo:-
Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.
Washindi wengine katika tuzo hizo ni hawa wafuatao:
Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili vya
Tanzania- Bora Mchawi - Dar Bongo
Massive.
Msanii Bora Chipukizi - Young Killer.
Wimbo Bora wa Zouk kwa 2014
- Yahya by Lady Jaydee.
Wimbo Bora wa Afro Pop - Number One by Diamond Platinumz.