Kama wewe ni mpenzi wa movie, Trailer ya kwanza ya movie ya The Expendables 3 tayari limetoka na kuwekwa mitandaoni kuashiria ujio rasmi wa movie hiyo.
Ndani yake muigizaji mkongwe Harrison Ford ameongezwa akiwa na waigizaji wengine wakali kama Antonio Banderas, Mel Gibson, Kelsey Grammer, Kellan Lutz, Victor Ortiz, na Ronda Rousey.
Ford anachukua nafasi ya Bruce Willis, ambaye ameripotiwa kutaka kiasi cha dola milioni 4 kwa ajili ya kucheza vipande vyake ambapo Sylvester Stallone hakufurahishwa na kitendo hicho.