Wakati macho na masikio ya dunia yote yakiwa kwenye soka hasa kwa kipindi hiki cha kombe la dunia sasa inshu imekuwa tofauti kwa kampuni ya Beats by Dr.Dre ambayo headphone zake zimepigwa marufuku kutumika kwenye kombe la dunia.
kampuni ya Beats Electronics ilitoa tangazo la luninga lililokuwa na dakika 5 ambalo walilipa jina la ‘Tittle the Game before the Game’.
Katika tangazo hilo wapo mastar kadhaa wa mpira wa miguu kwa msimu huu akiwemo mchezaji nyota toka Brazil Neymar Da Silva Santos Júnior,Mchezaji wa Spain Francesc “Cesc” Fà bregas pamoja na mchezaji kutoka Uruguay Luis Alberto Suárez DÃaz pamoja na Lil Wyne.
Unaambiwa baada ya FIFA kuliona hilo tangazo wamewakataza wachezaji wote kuvaa headphones hizo za Beats by Dre wakiwa kwenye viwanja hivyo vya kombe la dunia pamoja na sehemu zote za sherehe zitakazowahusisha pia waandishi.
Dili limeidondokea kampuni ya Sony ambao ni Official Partner na FIFA ambao wameahidi kuwapatia wachezaji hao headphones za kuvaa kwa kipindi hicho cha kombe la Dunia na hawataruhusiwa kuvaa aina nyingine yoyote ya headphone.
Cheki Tangazo lenyewe hapa...