Mtayarishaji wa muziki Tanzania Luciano Lucci Tsere aka Lucci Da Don ameamua kufunguka na kuhoji juu ya anavyouchukulia uamuzi mzuri wa rais Jakaya Kikwete kumleta mwanamuziki Usher Raymond pamoja na Terrence J Tanzania kwa ajili ya kutoa semina kwa wanamuziki wa Tanzania kuhusu muziki.
Lucci ameandika kupitia Twitter ambapo alianza kwa kumpongeza rais Kikwete lakini hakusita kusema kuwa ana maswali kadhaa kuhusu hatua hiyo.
“Big up to you Mheshimiwa Rais @jmkikwete for the effort you are making for our nation’s artists. However; I have a few queries”
Lucci amehoji “What have WE artists done with the knowledge WE have FREQUENTLY received from our own institutions such as BASATA and COSOTA? @jmkikwete”
Akimaanisha namnukuu “Sisi kama wasanii tumefanya nini na elimu ambayo tumekuwa tukiipata kutoka kwa taasisi zetu za muziki za hapa nyumbani kama BASATA and COSOTA?”
Lucci aliongeza kuwa “Kuna msemo “He who is faithful with little can be entrusted with much”…Je, Mheshimiwa @jmkikwete , have we been faithful with the little?”
Akimaanisha “Yule mwenye imani na kidogo anachopata anaweza kuongezewa zaidi lakini Je, Sisi tumekuwa na imani na hiki kidogo?”
Anyway, nisije nikapigwa mawe. I sure do hope this time we can actually apply what we are taught by these great music industry folk coming.
Mtayarishaji huyo wa muziki aliyetengeneza ngoma kali zikiwemo za mwanamuziki Cpwaa alimalizia kwa kusema kuwa “Anyway, nisije nikapigwa mawe. I sure do hope this time we can actually apply what we are taught by these great music industry folk coming.”
Akimaanisha “Anyway, nisije nikapigwa mawe. Ila nina imani kuwa safari hii tunaweza kutumia vilivyo kile tutakachofundishwa na watu hawa muhimu kwenye muziki wanaokuja nchini.”