Ukikamilisha dili la dola billion 3 utafanya kitu gani cha kwanza kabisa kutokana na hizo pesa ulizopata. Majibu yanaweza kuwa ni mengi kutokana na mawazo ya kila mtu.
Dr Dre ambaye amekamilisha dili la kuuza ya Beats kwa kampuni ya Apple ametumia zaidi ya dola million 40 kununua jumba la kifahari kutoka kwa modo tajiri Gisele Bundchen.
Jumba hilo lina vyumba vya kulala 8, sehemu 6 za kuegesha magari, mabafu 9, gym,bwawa kubwa la kuogelea,maporomoko ya maji na sehemu nyingine. Jumla eneo zima la nyumba lina square feet karibia 14,000.
Hicho ndicho alichofanya Dr Dre baada ya kupata pesa nyingi kutokana na dili la Beats, wewe ungefanya nini?