Macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha na matumaini ya Tanzania yalikuwa kwa kijana wa nyumbani, Diamond Platnumz ambaye ameingia katika tuzo hizo kwa mara ya kwanza.. Diamond aliteuliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele viwili, Best Male artist, na Best collaboration Song. Bahati haikuwa njema sana kwani Diamond hakufanikiwa kupata tuzo hizo..
Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’.
Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia Television.