Miaka kadhaa nyuma ziliwahi kutoka stori kuwa wanamuziki wengi wa Tanzania wanapoenda kufanya show nje mara nyingi hawapigi show kwenye club kubwa na taarifa hiyo iliunganishwa na maneno kuwa muziki wa Tanzania bado haujawa na nafasi ya kuwa na mashabiki wengi.
Kwa picha kadhaa ambazo wasanii wanapost kwa sasa wanapokuwa kwenye show zao nje ya nchi utaungana nami kwa kuamini kuwa muziki wa Tanzania umekua kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba umekaa kwenye ramani inayotambulika kimuziki.
Diamond Platnumz ni miongoni mwa wanamuziki kutoka Tanzania ameendelea kutuwakilisha vizuri kwenye majukwaa ya nje ya nchi,cheki jinsi wakazi wa Belgium walipopata nafasi ya kushuhudia show ya Diamond Platnumz.