Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.