Blogger Widgets

Wednesday, March 11, 2015

TAARIFA JUU YA AJALI YA BASI ILIYOTOKEA IRINGA LEO..!

ABIRIA zaidi ya 40 wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi la Majinja Express ambalo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kufunikwa na kontena maeneo ya Changalawe, Mafinga mkoani Iringa muda huu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita lori ndipo walipodondokewa na kontena hilo.
Inadaiwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria 65 na abiria nane tu ndiyo walionusurika katika ajali hiyo mbaya.

Taarifa ambayo kwanza ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya basi la abiria na lori la mizigo, kipindi cha Leo Tena Clouds FM wameongea na mashuhuda kutoka eneo la Changarawe, Iringa ambapo wamesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kuna idadi kubwa ya watu ambao wamefariki.
Mashuhuda wamesema basi la Majinja lilitokea Mbeya kuja Dar es Salaam limegongana na lori la mizigo katika eneo hilo, abiria waliofariki ni wengi japo idadi kamili haijafahamika.
image-11-03-15-03-30
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, kwa sasa yuko njiani kuelekea eneo la tukio ili kuona mazingira ya ajali na kutoa taarifa kamili.