Hii ilianza kuchukua Headlines jana April 03 kuhusu ishu ya ajali ambayo walipata mashabiki wa Timu ya Simba waliokuwa wakisafiri kwenda Shinyanga kushabikia Timu yao ambayo itakuwa ikipambana na Kagera Sugar leo April 4.
Leo imetawala pia katika vyombo vya Habari, Ripota wa Clouds FM Morogoro aliripoti tukio hilo, amesema ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya Morogoro ambapo mvua inaendelea kunyesha, utelezi wa Barabarani ukafanya gari hiyo kupata ajali.
Watu saba wamefariki na wengine 18 ni majeruhi ambao walipelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.