Leo June 08 2015 kulikuwa na mdahalo wa Wagombea wa Urais TZ ambao wanawakilisha CCM.. Mdahalo ulianza saa moja jioni Hyatt Regency Dar lakini Wagombea wengi hawakufika aliyefika ni Mgombea mmoja tu, Balozi Amina Salum Ali, wapo waliotoa sababu za kutofika lakini wengine hakukuwa na taarifa yoyote.
Ali Mufuruki ni mwenyekiti wa Waandaaji wa Mdahalo huo, hiki ndio alichokisema baada ya kutokea kwa hali hiyo. ”Tumesikitika kwamba wamejitoa.. Hiki ni kitu ambacho kimetuchukua muda mrefu sana kukiandaa. Sijui na sijapata nafasi kuzungumza nao nini kimewakuta“
“Tarehe 18 kutakuwa na mdahalo wa watu wa UKAWA… Hatuwezi kuwalazimisha kuja, wakiamua kutokuja hatuwezi kufanya chochote“
“Mzee Sumaye anauguliwa kwa hiyo hakuwepo hapa mjini… Mheshimiwa Nyalandu alithibitisha kushiriki leo asubuhi lakini ameenda Mbeya kikazi na leo usiku atasafiri kwenda nje ya nchi”
“Kinana alifafanua kuhusu hili jambo kwamba kila mtu ana hiari ya kuhudhuria ama kutokuhudhuria. Sidhani kama kuna tatizo kwenye chama… Sijapewa sababu ya hawa ambao hawajahudhuria”