Friday, February 20, 2015

VIDEO: Cheki "Behind the Scenes" Ya Video mpya ya Diamond na Linex

Hizi ni clip za utengenezwaji wa Video mpya ya Diamond na Linex.. Behind the scenes.. Jionee hapa.. Video inatengenezwa na Adam Juma..

 

TAARIFA YA MSIBA WA MSANII WA BONGO FLEVA, MEZ B

Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
MEZ-B2
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarifu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Noorah, Dark Master na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.

BRAND NEW AUDIO: Jux - Nikuite Nani. Sikiliza na Download hapa..

Hii Ndio Track mpya kutoka kwa Jux,, Wimbo unaitwa Nikuite Nani, Umetengenezwa AM Records..

Thursday, December 11, 2014

BRAND NEW AUDIO: JOH MAKINI FT G.NAKO XO

.
.
Hii ni single mpya ya msanii wa Hip Hop kutokea 87.9 (ArushaCloudsFM)  mwamba wa Kaskazini Joh Makini wimbo unaitwa XO akiwa amemshirikisha G Nako.
Isikilize hapa mtu wa nguvu kisha usisahau kuniandikia ya moyoni ili Joh Makini na G Nako wakipita hapa wasome kutoka kwa watu wao wa nguvu..
Bonyeza hapa kuingia kuisikiliza na kudownload moja kwa moja…. >>>> HAPA
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Monday, December 8, 2014

BRAND NEW VIDEO: G-nako Moralle..

Kutoka Kwa G-Nako WaraWara, hii ndio video yake mpya yaMoralle,, Video imefanyika Arusha, na ni moja kati ya zile Video Tano walizoahidi Weusi.. Kesho, December 9, itakuwepo hewani video ya Joh-Makini I see me.. stay with us..



HII NDIO TWEET YA DAVIDO ILIYOMKOSANISHA NA WATANZANIA..

dvdUsiku wa December 07 Tanzania imechukua tena headline kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hii ni baada ya Mtazania Idris kufanikiwa kushinda kwenye shindano la Big Brother Hot Shot 2014.
Usiku huo huo baada ya ushindi wa Idris,Diamond alipost tuzo aliyoshinda Nigeria baada ya matukio hayo kufanyika,Hit Maker wa single kadhaa ikiwemo Skelewu Davido alipost kitu ambacho kimezua tafsiri tofauti tofauti.
Post ya Davido ilisomeka >>’N they Cheat again lol’ baada ya muda mfupi post hiyo aliifuta ambayo bado Watanzania wamekua na maswali tofauti kuhusu hicho alichokiandika.
1DVD
Post hii ya kejeli, ambayo Davido aliipost kwenye ukurasa wake wa twitter, imemsababishia kujenga uadui na watanzania, na kuambulia matusi yakutosha kwenye social medias hususan kwenye Instagram.

HII NDIO TUZO NYINGINE ALIYOCHUKUA DIAMOND HUKO NIGERIA..

tuzoDiamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine ambayo hizi zilikua zikitolewa Lagos nchini Nigeria ambazo hizi hazikuwa na utaratibu kama wa tuzo zingine kwa kupiga kura.
Baada ya kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kupokelewa na Meneja wake Salaam,Diamond alipost maneno haya>>’Thanks God,we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#samenight Thank you Allah’
Tuzo hizi zinaitwa The Future Awards Prize in Entertainment ambapo kipengele alichokuwa akiwania Diamond alikuwa na wakali mbalimbali akiwemo Panshack au Ice Prince jina lake la zamani wa Nigeria na Michael Kwesi wa Ghana.
dngria

TANZANIA YAKIMBIZA TENA BIG BROTHER AFRICA..

IdrisLeo ni siku ya 63 tangu yaanze mashindano ya Big Brother Africa, ndiyo siku ambayo imefanyika fainali ya #BBAHotshots kwa mwaka huu 2014.
Labda nikukumbushe kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee iliyokuwa imebakiwa na mshiriki wake ndani ya Jumba la BBA katika ukanda wa Afrika Mashariki na tuliona namna ambavyo mastaa wengi wakitoa support kubwa kwa mshiriki huyo ambaye ni Idris.
Hatimaye usiku huu wa Desemba 07 historia nyingine imeandikwa Afrika, ambapo mwakilishi huyo kafanikiwa kuibuka mshindi

Tuesday, December 2, 2014

BRAND NEW AUDIO: Kala Jeremiah ft Nuruwell Usikate tamaa




HAWA NDIO WACHEZAJI WATATU WALIOTAJWA KUWANIA BALLON D'OR

FIFA Ballon d'Or Gala 2012
Orodha ya wachezaji watatu waliongia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Ballon’Dor inayotolewa kwa mchezaji bora wa dunia imetajwa hii leo .
Orodha hiyo imewajumuisha wachezaji watatu ambao ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo  , nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, na Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo  mwaka jana.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo mwaka jana.
Mchezaji ambaye anatetea tuzo hii hadi sasa ni Cristaino Ronaldo ambaye aliitwaa kwa mwaka 2013 na kwa jinsi mambo yanavyokwenda ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo mwakani .
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon'Dor.
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon’Dor.
Mshindi wa tuzo hii atatangazwa kwenye hafla itakayofanyika huko Zurich januari 12 ambapo tuzo mbalimbali zitatolewa .
neur
Kipa wa Ujerumani Manuel Neur atawania tuzo hiyo dhidi ya Lionel Messi na Cristaino

CHEKI PICHA,, HII NDIO AJALI ILIYOMHUSISHA DAVID BECKHAM..!!

becks 2
Moja kati ya story zilizoshtua wapenda michezo nchini England mwishoni mwa wiki hii ni ajali ambayo aliipata nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England David Beckham .
Becks alipata mkasa huo wakati akiwa anatoka kumchukua mwanae anayefahamika kwa jina la Brooklyn toka kwenye mazoezi ya kila siku ya timu yake ya Arsenal .
Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Gari ya Beckham aina ya Audi iligongana na gari nyingine ndogo na star huyo alipata jeraha kwenye bega lake japo halikuwa jeraha kubwa sana .
Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Mtoto wa star huyo Brooklyn amabye ni mchezaji wa timu ya Vijana ya Arsenal hakuumia kwenye ajali hiyo ambayo magari yote yaliyohusika yaliharibika vibaya .
Picha inayoonyesha familia nzima ya Beckham akiwa na mkewe Victoria Beckham na wanae wa kiume Brooklyn , Romeo na Cruz.
Picha inayoonyesha familia nzima ya Beckham akiwa na mkewe Victoria Beckham na wanae wa kiume Brooklyn , Romeo na Cruz.

Thursday, November 13, 2014

BREAKING NEWS: Msanii wa HipHop Geez Mabovu afariki Dunia..

Geez Mabovu
Geez Mabovu ni ambae hajavaa shati.
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2

Friday, November 7, 2014

MPYA HII KUTOKA WHATSAPP,, WAONGO SASA BAASI..

whatsapp-doble-checkNakumbuka moja ya taarifa kubwa zilizowahi kuchukua headlines mwezi Februari 2014 ilikuwa ni stori ya kuuzwa kwa mtandao wa Whatsapp kwa mmiliki wa Facebook, leo kuna taarifa nyingine mpya kuhusiana na watumiaji wa mtandao wa Watsapp.
Haya ni mambo manne mapya ambayo huenda hujayasikia kuhusu WhatsApp;-
1. Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
2. Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
3. Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
4. Ukibonyeza ujumbe uliotuma utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
whatsapp
Kuanzia jana huduma hiyo itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Ukibonyeza ujumbe wenyewe itakuonyesha muda ambao uliyemtumia ujumbe huo kausoma.
Tazama video hii uone mabadiliko hayo.