Blogger Widgets

Friday, August 30, 2013

Na hii ndio hatua ya makundi UEFA!!!

...

DIAMOND AMSHANGAZA MZEE GURUMO!!

Msanii  wa muziki wa kizazi kipya nchini, Maaruf kama Diiiamond Platnumz, Aliwaacha watu midomo wazi katika uzinduzi wa video yake mpya, Baada ya kumzawadia Mzee Gurumo, mwanamuziki wa miaka mingi na mkongwe aliyetangaza kustaafu mziki siku chache zilizopita zawadi ya Gari aina ya "Fun Cargo" Tukio hilo limetokea usiku huu ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji la DSM ambapo Diamond Platnum anazindua video yake mpya huku Kiingilio...

Thursday, August 29, 2013

DAH! 'BEEF' YA KAGAME NA RAIS WA TANZANIA IMEFIKIA HAPA!!!

RAIS Paul Kagame wa Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete.Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa Rwanda kususia kikao na kutoka nje...

Monday, August 26, 2013

YALIYOMO kwenye MAGAZETI YA LEO, Monday, August 26, 2013

...

SPORTS: Real Madrid and Tottenham have agreed a world record £86 million deal for Gareth Bale!

Spurs chairman Daniel Levy finally accepted the Spanish giants’ offer on Sunday and official confirmation of the transfer is expected in the next 48 hours.The clubs have come to an agreement on a straight cash deal to be paid in three installments, as Bale becomes the most expensive player in history, eclipsing the £80m Real paid Manchester United for.... >>Read More<&l...

Sunday, August 25, 2013

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Viongozi wengine wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Iringa!

Mwenyekiti Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa la kuzidisha muda wa mkutano.Polisi wanasema mkutano ulimalizika saa 12.30 badala ya saa 12.00Source: Jamii Forums  Swali lwa msingi kwa Polisi, sheria gani wanayotumia katika suala hili. Au ni ule mwendelezo wa kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa.Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Jeshi la...

Thursday, August 22, 2013

YALIYOMO KWENYE MAGAZETI YA LEO,, Thursday, August 22, 2013

...

Tuesday, August 20, 2013

PICHA: Hivi ndivyo hali ilivyokuwa Jijini Mwanza Jana!!

...

Monday, August 19, 2013

HIVI NDIVYO YULE TRAFIK FEKI ALIVYOANZA KAZI!!!

SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari 'feki' wa Usalama Barabarani mwenye cheo cha Sajini, akifanya kazi ya kuongoza magari eneo ya Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam, mambo mapya yamezidi kubainika juu ya sababu za mtu huyo kujiingiza katika kazi hiyo bila kutambuliwa na Jeshi la Polisi. Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya kuaminika, zinasema trafiki huyo 'feki', ambaye inadaiwa jina lake halisi ni James Juma Hussein (45),...

Sunday, August 18, 2013

Waislamu Msikiti wa Mtambani ‘Wamteka’ Askari Polisi!!

BAADHI ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani Jijini Dar es Salaam jana wamemkamata mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi na kumshikilia kwa muda kabla ya kumwachia kwa masharti kadhaa. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kimebainisha askari aliyekamatwa ni Jonathan Tossi ambaye anafanya kazi kitengo cha habari na uhusiano wa Jeshi la Polisi. Polisi wakizunguka eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani. Askari...

MWAKYEMBE AWAANIKA WALIOMSAIDIA MASOGANGE KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA AIRPORT!!!

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana ameanika majina ya watu saba waliohusika kupitisha mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja. Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa wa Idara...

Wednesday, August 7, 2013

Mfanyabiashara Maarufu wa Madini Auwawa kwa kupigwa Risasi Arusha!!

ARUSHA: Mfanyabiashara maarufu wa madini Mererani na Mmiliki wa SG RESORT ya Arusha, Bw. Erasto Msuya ameuwawa leo majira ya alasiri wakati alipokuwa akitokea Mererani kuelekea Moshi. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana mara baada ya tukio hilo zinasema kuwa mfanyabiashara huyo alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mara baada ya majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya barabara ya kia. inasemekana wauaji wamekimbia...

Monday, August 5, 2013

WANAFUNZI 8000 WAKWAMA KUJIUNGA VYUO VIKUU NCHINI!!!

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imekataa majina ya wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza kwenye fomu za waombaji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU  Profesa Sifuni Mchome, wanafunzi hao hawakuchaguliwa na tume hiyo kujiunga na vyuo vikuu kutokana na maombi yao ya programu zote walizochagua kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa. Taarifa hiyo ilieleza kuwa sababu za kutochaguliwa...

Jaji Francis S.K. Mutungi ateuliwa kuwa msajili wa vyama vya siasa!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa...