Blogger Widgets

Friday, December 6, 2013

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia..

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.

Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kuwa mwanawe wa kume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004.

Tuesday, December 3, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA VIN DIESEL KUFUATIA KIFO CHA PAUL WALKER..!

Paul Walker, Vin Diesel
Paul Walker and Vin Diesel

"To live in the hearts we leave behind, is not to die," the actor quoted Thomas Campbell on his Facebook page in speaking out for the first time about the death of longtime friend Paul Walker, his costar in four of six films in the Fast and the Furious series.
They were on a break from shooting the latest installment of the series when Walker waskilled in a single-car crash Saturday, along with the driver of the vehicle, Roger Rodas.
"Pablo, I wish you could see the world right now... and the profound impact, your full life has had on it, on Us... on me..." Diesel wrote.
"I will always love you Brian, as the brother you were... on and off screen."
Walker first played Brian O'Conner, undercover cop-nemesis turned ally of Diesel's Dominic Toretto in 2001's The Fast and the Furious, the original film in the hit action franchise that has since gone on to earn more than $2 billion worldwide.
Vin Diesel, Paul Walker, Fast and the Furious






















Production on Fast & Furious 7 has been delayed for the time being while they figure out how to handle Walker's tragic absence. Leaked footage of the funeral of Sung Kang's Han and Gal Gadot's Gisele (the action apparently picks up after the events in The Fast and the Furious: Tokyo Drift) briefly made it online before being yanked down by the studio. (E! Online and Universal Studios are both members of the NBCUniversal family.)
Diesel joins castmates including Tyrese, who wept at the scene of the crash site in Santa Clarita, Calif.; Jordana Brewster, who played Walker's love interest in the series;Michelle Rodriguez; and Dwayne Johnson in paying individual respects to their fallen friend and colleague.
"Paul was an enormous presence in my life for the past fourteen years," Brewster said in a statement. "While many would be satisfied with material success it made Paul more convinced of the need to help others...I don't know anyone who lived each moment more fully and loved life more than Paul; making his loss all the more heartbreaking."
Johnson told Entertainment Weekly, "The most important thing that we had in common was the importance of family time and being a great father to our daughters. We bonded over that."
Source: E-online

Sunday, November 24, 2013

Mama Yake Zito afurahia mwanae kuvuliwa uongozi, HAYA NDIO ALIYOYASEMA!!

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.
Mama+Zitto+Clip
“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.
Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru  dhidi ya.., >>Read More<<

Hivi Ndivyo P-SQUARE walivyoiteka Dar Jana!!!


























Taarifa ya CHADEMA kwa Watanzania kuhusu uamuzi wa kuwavua uongozi Zitto Kabwe na wenzake!

chadema
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20 Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013 imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.
Kwa mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye ‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango wa kuipasua pasua CHADEMA na kuiangamiza kabisa kwenye uso wa siasa za Tanzania. Huu sio mkakati wa kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya Chama kwa njia za kidemokrasia na za kikatiba. Ni mpango wa kukiteka nyara Chama na kukiua. Ndio maana watunzi wa waraka huu wamesema kwenye waraka wao: “Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndio maana hata lugha iliyotumika ndani hapa ni ya pekee.” Kamati Kuu inaamini mkakati wenye malengo halali ya kufanya mabadiliko ndani ya Chama kwa njia halali za kikatiba usingependekeza kwamba: “Vikao vyetu na yeye (MM aka Mhusika Mkuu aka Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe) vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.” Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba kama mkakati huu ungekuwa na malengo mazuri ya kukijenga Chama na sio kukiteka nyara na kukiua, wanamtandao hawa wasingependekeza utaratibu ufuatao wa utekelezaji wa mpango: “M1 (Dk. Mkumbo) ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa.”
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichana chana Katiba ya Chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya Chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba. Wakati ibara ya 10.1(iv) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama ambazo ni sehemu ya Katiba ya Chama chetu ya mwaka 2006 inamkataza kiongozi wa CHADEMA asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini, au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya Chama na miongoni mwa jamii kisiasa au kijamii”, wanaMtandao wa Ushindi wameonyesha wazi kuwa wanaendekeza siasa za udini kwa kusema yafuatayo juu ya waliemwita ‘mtu tunayemtaka’, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe: “Kwa kuwa ni Mwislamu, hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.”
Wakati ibara ya 10.1(viii) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka kila kiongozi wa CHADEMA “… kuwa mkweli na muwazi wakati wote … na aachane na vikundi vya majungu na wadanganyifu (rumour mongers) …”, wanaMtandao wa Ushindi wameeleza kwenye waraka wao kwamba mipango yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 ‘itafanyika kwa usiri mkubwa.’ Wakati ibara ya 10.1(ix) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama inamtaka “kiongozi asijihusishe na vikundi na vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”, wanaMtandao wa Ushindi wamesambaza tuhuma za uongo dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa (ambaye wanamwita kwenye waraka wao kuwa ni ‘Mpinzani wetu’) kuwa “… hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii…. Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi za chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.”
Wakati ibara ya 10.1(x) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka “kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Kanuni”, tuhuma zote zilizotolewa na wanaMtandao hawa dhidi ya viongozi wakuu wa Chama chetu hazijawahi kutolewa na yeyote kati ya wanaMtandao hawa katika kikao chochote halali cha Chama cha ngazi yoyote.
Wakati ibara ya 10.1(xii) ya Kanuni za Uendeshaji inaeleza kwamba “itakuwa marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu Chama, kiongozi au mwanachama yeyote wa Chama …”, Mkakati wa Mabadiliko 2013 umejaa kashfa kubwa, matusi mengi na udhalilishaji mkubwa wa Chama, viongozi wake wakuu na wanachama kwa ujumla. Hivyo, kwa mfano, Mwenyekiti wa Chama Taifa ametuhumiwa na wanaMtandao hawa kuwa ni mtu mwenye ‘uzalendo unaotia shaka’, mwenye ‘elimu ya magumashi’, ‘mzito kujieleza’, ‘mtu mwenye akili ndogo’, n.k.
Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Hakuna chama au taasisi yoyote duniani inayoweza kunyamazia mkakati wa aina hii dhidi yake na viongozi wake wakuu na ikadumu au kubaki salama. Chama au taasisi yoyote inayoendekeza vitendo vya aina hii miongoni mwa viongozi wake wa ngazi yoyote au miongoni mwa wanachama wake wa kawaida inakaribisha kifo na mauti. Chama chetu na viongozi wake wa juu wamekaa kimya kwa muda mrefu sana; wamevumilia mashambulizi na kashfa nyingi sana dhidi yao binafsi na dhidi ya Chama; wamestahimili matusi makubwa sana dhidi yao. Chama chetu kimevumilia yote haya na viongozi wake wamevumilia yote haya sio kwa sababu walitaka Chama chetu kiuwawe na wanaMtandao hawa. Uvumilivu wote huu ulitokana na haja ya kuwapa wanaMtandao wa Ushindi fursa ya kugundua hatari ya siasa zao na kuwapa muda wa kujirekebisha na kujirudi.
Kama ilivyo kwa binadamu au taasisi yoyote ile, uvumilivu wa Chama chetu na viongozi wake wakuu una kikomo. Na hiki ndio kikomo cha uvumilivu wa Chama chetu, viongozi wake na wanachama wake kama wanavyowakilishwa na Kamati Kuu ya Chama chetu. Hivyo basi, katika kikao chake tajwa, Kamati Kuu ya Chama chetu, kwa kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya dharura chini ya ibara ya 6.5.2(d) ya Katiba ya Chama, imeazimia yafuatayo kuhusu Mkakati wa Mabadiliko 2013 na hao wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi:
Kwamba, kuanzia sasa, viongozi wote waliohusika ama kuhusishwa na mkakati huu, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba wavuliwe nyadhifa zao zote za uongozi ndani ya Chama; Kwamba timu ndogo ya pamoja ya watendaji wa Sekretariat ya Makao Makuu ya Chama na wajumbe wa Kamati Kuu ifanye uchunguzi wa haraka ili kumtambua mtu anayeitwa M2 na ambaye anadaiwa kuwa mtumishi wa Makao Makuu ya Chama ili hatua stahiki na za haraka zichukuliwe dhidi yake, pamoja na watu wengine wote watakaobainika kuhusika na mpango huu wa uhaini dhidi ya Chama chetu; Kwamba Kamati ya Chama ya Wabunge inaelekezwa kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe anavuliwa madaraka yake yote kama Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, with immediate effect;
Kwamba viongozi waliotajwa katika aya ya (a) waandikiwe hati zenye tuhuma dhidi yao haraka iwezekanavyo na watakiwe kujieleza kwa nini wasifukuzwe kwenye Chama kwa vitendo vyao na wapatiwe fursa kamili ya kujitetea kama inavyotakiwa na ibara ya 6.5.2(a), (b) na (c) ya Katiba ya Chama; Kwamba mara baada ya utekelezaji wa azimio (d), Kamati Kuu ikutane kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatma ya watuhumiwa na hatua nyingine zitakazofuata; Kwamba waraka wa wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi uwekwe hadharani na usambazwe kwa vyombo vya habari vya aina zote ili wananchi wa Tanzania, wanachama na viongozi wa Chama chetu na dunia nzima kwa ujumla iweze kupima uzito wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 na uhalali wa maamuzi haya ya Kamati Kuu.
Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo waliiomba Kamati Kuu iwaruhusu kujiuzulu nyadhifa zao baada ya Mkakati wao wa kukiteka nyara Chama na kukiangamiza kujulikana mbele ya Kamati Kuu. Kwa kuzingatia uzito wa makosa waliyokifanyia Chama, viongozi wake wakuu na wanachama wake kwa ujumla; na kwa kuzingatia uzito na umuhimu wa nyadhifa kubwa walizo nazo ndani ya Chama; na kwa kuzingatia uelewa wao wa Katiba, Kanuni na taratibu za Chama na uzoefu wao katika safu za juu za uongozi wa Chama, Kamati Kuu ilikataa kwa kauli moja kuridhia maombi hayo ya kujiuzulu. Kufanya hivyo ingekuwa ni sawa na kuwaruhusu wajiondoe kwenye uongozi wa Chama wakiwa na heshima wasizostahili hata kidogo.
Chama chetu ni tumaini pekee la Watanzania wote wanaotaka mabadiliko ya kweli na ya kimsingi katika mfumo wa kiutawala, kiuchumi na kijamii wa nchi yetu. Hii ndiyo sababu kubwa na ya pekee iliyosababisha vita kubwa na chafu inayopigwa dhidi ya Chama chetu na viongozi wetu wakuu. Lengo kuu ni kuwachafua viongozi wakuu, kuleta mgogoro na mgawanyiko ndani ya wanachama, viongozi wake na hivyo kukichafua Chama mbele ya macho ya Watanzania. Chama chetu kikishachafuka kwa mtindo huu, matumaini ya Watanzania wanaotaka mabadiliko yatakufa. Vita hii kubwa haijaanza jana, na haitaisha kesho. Kama ambavyo tumekabiliana nayo na kuishinda siku za nyuma, vivyo hivyo tutakabiliana nayo mara hii na kuishinda. Kama Chama chetu kilivyoibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika mapambano ya siku za nyuma, vivyo hivyo Chama chetu kitaibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika awamu hii ya mapambano.
Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu wasife moyo, bali waendelee kukiunga mkono chama chao cha ukombozi. Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu waendelee kulilinda tumaini lao pekee la mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Badala ya kukatishwa tama, kila mmoja wetu aongeze bidii maradufu ili kuwashinda wale wanaotaka kuleta majanga katika Chama chetu na kwa Taifa letu.
——————————————
FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) – MWENYEKITI, TAIFA
——————————————
WILBROD PETER SLAA – KATIBU MKUU
Source: Chadema Blog

Saturday, November 16, 2013

Prof. Kapuya atishia kuishitaki JamiiForums...!

SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

Wednesday, November 13, 2013

MAGAZETI YA LEO,, Wednesday, November 13,

DSC 0025 28f7e
DSC 0026 56011
DSC 0027 8af2a
DSC 0028 9dfb1
DSC 0029 cee27
DSC 0030 3ad70
DSC 0031 a44c0
DSC 0032 84c27
DSC 0033 e36ab
DSC 0034 bbde8DSC 0035 f8388

Tuesday, November 12, 2013

BREAKING NEWS! Dk Sengondo Mvungi afariki dunia!!!

Habari za kusikitisha zilizotufikia jioni hii zinasema kuwa Dk. Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 mwaka huu kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Muhimbili kitengo cha MOI ambako muda wote alikuwa hajitambui baada ya kushambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya sehemu ya kichwani akiwa nyumbani kwake Kibamba. Wakati Dk. Mvungi anafariki, jana Jeshi la Polisi, kupitia  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, lilitangaza kuwakamata watuhumiwa 9 wakiwa na mapanga yaliyotumika katika uvamizi huo.

Marehemu Dk. Sengondo Mvungi  enzi za uhai wake.

Mpaka mauti yanamfika, Dk. Mvungi alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB).
Marehemu aliwahi kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.

Tuesday, November 5, 2013

BABU SEYA, PAPII KOCHA... KAZI IMEKWISHA

MABERE Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.
Babu Seya (wa pili kulia) na Papii Kocha (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani kusikiliza rufaa yao.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya ameimaliza, sasa anasubiri majaji waliosikiliza alichokisema ili watoe uamuzi wa mwisho lakini pia anamtegemea Mungu.
“Mimi kazi nimemaliza sasa nawasubiri hao wakubwa (majaji) ili wapime nilichowaambia kwa mujibu wa sheria na kisha watoe uamuzi, lakini pia namtegemea Mungu,” alisema Marando.
Alisema ameiomba Mahakama ya Rufaa Tanzania ifanye marejeo kuhusu hukumu iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani wateja wake hao na adhabu ya kifungo cha maisha jela wanayoitumikia kwa sasa.
Wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, Mabere Marando.
Alipoulizwa alitumia muda gani kuwasilisha hoja zake hizo, Marando alisema takriban dakika 120 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Salum Massati.
Akiwa mahakamani hapo, Marando alidai kuwa mahakama iliteleza katika kutoa uamuzi uliowatia hatiani na kuwafunga maisha wateja wake na kwamba kuteleza huko kunaonekana waziwazi.
Alifafanua kuwa wakati wakifanya majumuisho ya kesi hiyo, mahakama ilijiridhisha kwamba kulikuwa na makosa katika kupokea ushahidi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuata taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa watoto.
Alieleza kuwa mtoto anayesoma shule kuanzia ya msingi anapotoa ushahidi licha ya tahadhari, ana uwezo wa kutambua zuri na baya na kwamba lazima ushahidi wake uwekwe kwenye kumbukumbu ya maandishi na kwamba usipoonekana ushahidi wote ni batili na unaondolewa.
Babu Seya na Papii Kocha wakiwa na furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Katika shauri hilo upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka uliwakilishwa na Mawakili Jackson Mlaki, Angaza Mwaipopo, Emakulata Banzi, Joseph Pande na Apimack Mbarouk ambao waliyapinga maombi hayo kuhusu marejeo kwa madai kuwa yamepelekwa mahakamani bila usahihi.
Mahakama hiyo imesema itatoa uamuzi wake siku itakayotangaza.
Babu Seya na Papii Kocha wako jela kwa makosa 10 ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo.



Walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Aprili na Oktoba 2003 eneo la Sinza Kwaremy jijini Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, Mwalimu wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye alishitakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa hayo kwa kuwaruhusu baadhi ya wanafunzi hao kutoka madarasani, aliachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.

Wednesday, October 23, 2013

SHULE ZA SEKONDARI NCHINI KUUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO..!!

0002_1ab10.jpg
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ukianzia Shule ya Kambangwa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Meneja wa Samsung Tanzania Kishor Kumar, wapili ni Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom, Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng'wigulu.
0003_8d170.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung. Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng'wigulu, na Mtaalamu wa komputa wa Samsung, Julius Giabe.
0004_05253.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame, akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo wa taifa wa mawasiliano, uliofanyika kwa kuanzia na shule ya Msingi Kambangwa ya jijini Dar es Salaam.
0005_d4b71.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung. Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, na Mtaalamu wa komputa wa Samsung, Julius Giabe.
0006_217d7.jpg
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kambangwa, wakitoa burudani kwa wageni waalikwa, Wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari na Mkongo na Taifa wa Mawasiliano.(P.T)