Blogger Widgets

Sunday, September 29, 2013

Na hivi ndivyo Magaidi walioshambulia Westgate walivyofanikiwa kutoroka..!!

Video hii inaonesha jinsi gani Magaidi wanaoaminika kuwa wafuasi wa kikundi cha Alshabab walivyofanikiwa kutokomea baada ya kufanya Mauaji ya kutisha Westgate Mall jijini Nairobi.
Njia hii ambayo inaaminika magaidi hao waliitumia, imegunduliwa na Kikosi cha wanausalama cha Kenya siku ya Jumanne ambapo ni Siku nne baada ya tukio lenyewe..


Saturday, September 28, 2013

MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA


Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na


MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

Thursday, September 26, 2013

Huyu ndio mtoto wa miaka minne aliyeokoa Maisha ya Mama yake kwenye Shambulio la Westgate..!!!

Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.

Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuumizwa na maneno hayo, magaidi hao walimpa Elliott pamoja na dada yake mifuko miwili miwili ya chokleti na kuwaomba msamaha.
Taarifa hizo zinasema kuwa,  gaidi huyo alisema “Samahani nisamehe, sisi siyo watu wabaya”.
Mama huyo anasema kuwa, kabla ya kukamatwa na magaidi hao, yeye na watoto wake walikuwa wamejificha kwenye jokofu la kuhifadhi nyama lililopo ndani ya duka la Nakumatt kwa zaidi ya saa moja na  nusu.
Anasema kuwa, baada ya kukamatwa na magaidi hayo, walimpiga risasi ya paja.
Mjomba wa watoto hao aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa  “Walikuwa na bahati kuweza kutoka kwenye mikono ya hao magaidi. Hao magaidi walisema kuwa, kama kuna mtoto yeyote aliye hai ndani ya jengo hilo wanaweza kuondoka.
‘Mama yao alisimama na kusema ‘ndio’ , binamu yangu aliweza kupata ujasiri wa kusimama na kuwaambia kuwa, nyie ni watu wabaya sana’.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya magaidi hao kujua kuwa mama huyo na watoto wake hawakuwa kati ya watu waliowalenga, hawakuwaua.

Ufugaji wa aina hii Handeni haukubaliki..!!

Leo naomba tuachane na habari zetu za historia na utalii. Ninataka kuzungumzia uharibifu wa mazingira kama nilivyoshuhudia huko Handeni mkoani Tanga katika Kijiji cha Nyasa, vitongoji vya Kariakoo na Ubungo.
Ng’ombe wakiwa Hifadhi ya Msitu wa Nyasa, kitongoji cha Ubungo. Picha ya Maktaba. 
Maeneo hayo yanaendesha shughuli za ufugaji, kilimo na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Awali eneo hilo lilikuwa ni hifadhi ya msitu, likaondolewa katika hifadhi ya msitu, lakini kwa kweli uchimbaji wenyewe na ufugaji unaharibu mazingira kwa kasi ambayo kama haitadhibitiwa mambo hayatakuwa mazuri katika siku za usoni.
Eneo hilo limevamiwa na wafugaji ambao wanalisha mifugo yao bila kujali kwamba wanaharibu ardhi, uoto wa asili na kusababisha  jangwa. Wanyama hao wanalishwa hovyo, unapowaona utadhani umekutana na makundi ya nyati katika mbuga za wanyama.
Nilishawahi kuandika wakati fulani kuwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji unatakona na kuendekeza aina ya ufugaji ambao hauzingatii maarifa na teknolojia ya kisasa.
Tulipowaona ng’ombe hao moja ya wazo ni kuwa unaweza kuwadhibiti wasiingie kwenye mashamba ya wakulima kama wanalishwa kwa makundi makubwa ya ng’ombe 300  au zaidi.
Serikali inapaswa kuachana na maneno matupu kuhusu kuingiza maarifa ya kisasa katika shughuli za kilimo na ufugaji. Handeni katika msimu uliopita kulikuwa na tatizo la njaa na moja ya sababu ni kukosekana kwa mvua za kutosha.
Ufugaji wa kuharibu misitu na mazingira ya maji unaoendeshwa huko hauwezi kuwa rafiki ila kuongeza tatizo lingine ambalo limekuwapo huko kwa muda mrefu.
  Inashangaza sana kwa Serikali kuwa wawekezaji wakubwa wanapotaka kufanya shughuli za uchimbaji, Baraza la Taifa la Mazingira (Nemc) linawasimamia, lakini Nemc hiyo hiyo inanyamaza kimya pale wahusika wanapoharibu mazingira hasa  wachimbaji wadogo.
Source: Mwananchi

Tuesday, September 24, 2013

Na hizi ndio kurasa za mbele za magazeti ya leo,, Jumanne, 24,September!










Kodi ya sim card sasa kuanza mara moja!

Mamlaka ya mapato nchini(TRA) imeandika waraka kwenda kwa makampuni ya simu nchini kuagiza kuanza utekelezaji wa kukata kodi ya laini ya simu.Kodi hiyo ni kuanzia July 30 mpaka september mwaka huu.Hii ina maana kwamba kila mtumiaji atakatwa sh 3000 ikiwa ni kodi ya mwezi July,August na September.Kwa maana hiyo mwenye laini mbili atakatwa sh 6000 na mwenye laini tatu atakatwa sh 9000.

Na katika hatua nyingine wateja milioni 8 simu zao kufungwa.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Tanzania Daima

source:TANZANIA DAIMA

Monday, September 23, 2013

Picha zinazosadikika kuwa ni za Wanamgambo wa Alshabab Wakiwa ndani ya Westgate Mall..

Suspected AlShabaab fighters inside Westgate. Look how comfortably they are walking around as if they're shopping ! pic.twitter.com/YURCpyNhzz

Picha ambayo bado haijashibitishwa ya al-Shabaab wanaofanya mashambulizi wakiwa ndani ya Westgate Mall


Tanzania yafuatilia raia wake Nairobi..!!

Wakati Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiahidi kuwasaka na kuwakamata walioua watu katika eneo la Westgate, Nairobi, Serikali ya Tanzania inawasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ili kufahamu kama raia wake walikuwa miongoni mwa watu walioathiriwa na shambulio hilo.

Watu 59 waliuawa na 107 kujeruhiwa wakati magaidi walipovamia juzi kwenye eneo la maduka jijini Nairobi.
Bado askari wa Kenya wakisaidiwa na maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na wale wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) wanapambana na magaidi hao. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, John Haule alisema jana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Batilda Buriani alikutana na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya lakini hadi jana hakukuwa na taarifa zozote za Watanzania kuwepo kwenye tukio hilo.
“Tunaendelea kuwasiliana na ubalozi wetu Nairobi kujua hali ilivyo, lakini hadi sasa hatuna taarifa rasmi kuhusiana na raia wetu kuwepo kwenye tukio hilo. Nimezungumza na balozi wetu ameniambia bado anaendelea kukutana na wenzetu wa Mambo ya Nje wa Kenya,” alisema Haule.
Akihutubia taifa kwenye Ikulu ya Kenya jana, Rais Kenyatta alisema Serikali yake haitarudi nyuma katika kupambana na ugaidi mahali popote, huku akisema ugaidi si tatizo la Kenya pekee, bali la kimataifa na kwamba litamalizwa kwa nchi kushirikiana.
“Tunatakiwa kuwa kitu kimoja na mpaka sasa Idara ya Usalama inaendelea kuimarisha ulinzi eneo husika, magaidi waliopo katika jengo ni kati ya 10 hadi 15. Tutashinda vita hii ya ugaidi kwa umoja wetu na tuweke tofauti zetu pembeni,” alisema.
Awali, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga aliwataka Wakenya kutokuifananisha vita ya ugaidi na udini wala ukabila na kusisitiza kuwa matukio kama hayo yametokea hata katika nchi za Ulaya.
“Mataifa ya kigeni yasisitishe safari za kutoka ndani na nje ya Kenya, tusigawanyike kwa njia yoyote ile,” alisema Odinga.

Sunday, September 22, 2013

Picha Zaidi za Shambulio la Kigaidi Kenya..!

 37
36
35

34

3338
32

32

31
30

Al shabaab wakiri kuhusika tukio la kenya, wadai Kenya ilipuuza onyo lao..!!

Afisaa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, amefahamisha BBC kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa Afisaa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.

Wanajeshi wa Kenya wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.
Afisaa mkuu wa mambo ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofariki ni kumi na moja lakini shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.
Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.
Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.
Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taharuki ilianza hii leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.
Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu , takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi au kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Source: BBC

Saturday, September 21, 2013

UPDATES NA PICHA ZA TUKIO LA UVAMIZI KENYA..!!
















Gunmen ambush Nairobi shopping mall, At least 20 killed,Red Cross says..

Gunmen ambushed an upscale shopping mall in the Kenyan capital on Saturday, leading to a fierce gunbattle with police and at least 20 people killed, the Kenyan Red Cross said.
Fifty more people were wounded in the attack at the mall in Nairobi, said Abbas Gullet, head of the Kenyan Red Cross.
The gunmen burst into the mall and shot indiscriminately, taking some people hostage, according to a senior Kenyan government source.
"All of a sudden we heard some shots and people rushing," said Zulobia Kassam, who was having coffee at the mall. "We realized we were under attack. We rushed to the back, trying to hide and we heard random shots from everywhere -- upstairs, downstairs."
She said they stayed in hiding for about 40 minutes before sneaking out through a back door.
"People were petrified, crying, praying," she said. "We were told there were hostages being held."
It was unclear how many hostages the attackers took, but police are trying to negotiate for their release and retake the building, according to the source.
Attackers appear to be of Somali origin, a Kenyan government source and Western diplomatic sources told CNN.
The military asked local media not to televise anything live because the gunmen are watching the screens in the mall.
Crowds fled down the streets as soldiers in military fatigues crawled under cars to get closer to the mall, guns cocked.
Surveillance helicopters flew overhead.
"We urge Kenyans to keep off Westgate mall, adjacent roads and its environs until further notice," the Interior Ministry said on its Twitter page.
It declined to release further information, saying it will issue a statement later.
"We're doing our job to ensure that everyone is evacuated to safety," the ministry said. "This is a scene of crime, let police do their job."
CNN affiliate NTV reported multiple shooters were at the scene and terrified shoppers were hiding inside the mall, which is popular among expatriates and the wealthy.
The high-end mall opened six years ago, and has more than 80 stores.
Source: CNN

Hakimu achomwa kisu mahakamani..!!

Shinyanga. Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.
Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.
Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.
Hata hivyo, baada ya kutoa maelezo, si mshtakiwa wala mdhamini wake aliyehudhuria mahakamani hapo licha ya kesi hiyo kusikilizwa mara mbili bila ya taarifa yoyote kabla ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo jana.
Kushambuliwa
Baada ya hukumu hiyo mlalamikaji alitoa shukrani na kuwashika mikono wote waliokuwamo mahakamani humo na kutoka nje.
Ilidaiwa kuwa baada ya dakika 15, Izengo alirudi mahakamani hapo na kudai kuwa ameleta risiti ya kumwonyesha hakimu thamani ya baiskeli yake alipoingia ndani ndipo kelele za Mshauri wa Baraza, Mary Wamba zikaanza kusikika akisema: ‘Njooni jamani hakimu kavamiwa anapigwa’.
Baada ya watu waliokuwa karibu kuingia katika ofisi ya Mahakama hiyo walikuta hakimu ameshacwhomwa kisu katika shavu la upande wa kushoto huku akivuja damu nyingi huku mtuhumiwa huyo akiendelea kumshambulia. Baada ya tukio hilo, wasamaria wema walimpeleka hakimu huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa matibabu.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema mtuhumiwa alikamatwa mara baada ya tukio hilo kusubiri hatua za kisheria dhidi yake.

Thursday, September 19, 2013

'Scandal' ya Unga Afrika Kusini,, Akina Masogange kuachiwa!!!

WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.

Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
“Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. Kama zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi. Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine, Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo katika kundi la dawa za kulevya.
Ni sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
Vyanzo vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa dhamana.
Kwa mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Gazeti hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
“Unapozungumzia vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.
“Mtu anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
“Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. Hiyo ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za Kichina.
Mwaka 1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Raia Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.
Hata hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
“Haya mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye thamani ile. Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa,” alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya.
- Source: Raia Mwema 

Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani.!!

Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini.
Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette alikuwa amemaliza muda wake nchini Kenya na alitakiwa kuja kuiwakilisha nchi yake Tanzania.

Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na Gazeti la Standard la Kenya akieleza kuwa anajipanga kurudi kwao baada ya kukataliwa na Serikali ya Tanzania.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ndio wanaoshughulika na hayo mambo, waulizeni.”
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema wizara yake haijapata taarifa za kukataliwa kwa balozi huyo.
“Suala hilo linahusu ofisi ya Rais, mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa na hata kama ingekuwapo hiyo taarifa siyo ya `public’.
“Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.
“Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine,” alisema Mkumbwa.
Alikariri Kifungu cha Nne cha Azimio la Vienna ambacho kinaruhusu nchi kukataa balozi wa nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
“Nchi inayopeleka balozi katika nchi nyingine inatakiwa kutoa jina mapema kwa nchi nyingine. Hata hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa kumkubali au kukataa uteuzi,” kinaelekeza kifungu hicho.
Source: Mwananchi

Tuesday, September 17, 2013

Kashfa mpya dawa za kulevya..!!

Raia wa Nigeria aliyefukuzwa Kenya miezi minne iliyopita kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, amekamatwa tena nchini humo akiwa na pakiti 425 za heroin, akiaminika kwamba alipitia Tanzania.

Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Enobemhe Emmanuel Peter inaaminika alishukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Nigeria na kisha kwenda Kenya kwa barabara, kupitia mpaka wa Namanga mkoani Arusha.
Peter alikamatwa pamoja na mwanamke ambaye ni raia wa Kenya, usiku wa Ijumaa iliyopita jijini Nairobi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
Raia huyo wa Nigeria ni kati ya wageni waliofukuzwa nchini humo Juni mwaka huu kwa agizo la Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliyeamuru raia wa kigeni wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wafukuzwe nchini humo.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha Kenya, Dk Hamisi Massa alisema uchunguzi zaidi wa dawa hizo utafanyika kabla mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani.
“Ni kati ya watu waliokuwa wamefukuzwa nchini katika nyumba aliyokamatiwa kulikutwa pia na pakiti 425 za heroin,” alisema Dk Massa.
Mtu huyo amekamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa zilizoonyesha kuwa, watu wengi waliofukuzwa Kenya kutokana na kujihusisha na biashara hiyo sasa wamerejea tena.
Julai 9 mwaka huu, Ofisa Uhamiaji wa nchi hiyo, Edward Kabiu Njau alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kumruhusu Anaeke Chimenze, aliyefukuzwa nchini humo, kurejea tena.
Chimenze ambaye ni raia wa Nigeria mwenye pasi ya kusafiria namba 02743350, pia anadaiwa kurudi nchini humo kupitia mpaka wa Namanga.
Uhamiaji Tanzania
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna, Abbas Irovya alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yupo nje ya ofisi. “Mtafute Tatu ndiye mtu wa habari zaidi, kama atakuwa amepata hizo taarifa atakueleza,” alisema.
Mwananchi ilipomtafuta Tatu Iddi alisema hajapata taarifa hizo na kutaka mwandishi amtumie barua pepe ikiwa na maelezo ya mtu huyo aliyekamatwa ili aweze kutafuta taarifa zaidi.
Source: Mwananchi

Chadema kumshitaki Balozi wa China UN..!!

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.

Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama.
Tukio la Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM lilitokea Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri kivuli wa mambo ya nje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana Jijini Mwanza, Ezekiel Wenje alisema Chadema wameamua kuchukua hatua hizo ili kukomesha vyama vya siasa kutumia mabalozi kama wawakilishi wa vyama vyao kwa kufanya uenezi kwenye mikutano ya siasa.
Wakati Wenje akisema hayo Katibu Mkuu Taifa wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema chama chake kinaangalia namna ya kumchukulia hatua za kumshtaki Balozi huyo akidai kuwa kitendo cha kushiriki siasa za CCM na kisha kuvalishwa kofia ya chama hicho ni kiunyume na taratibu za UN.
Kauli ya Dk Slaa aliitoa juzi jioni wakati akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe.
Kiongozi huyo yupo mkoani Mbeya akiwa ameambata na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akifanya mikutano maeneo mbalimbali lengo likiwa kuwaeleza wananchi wa Mbeya kuhusiana na kitendo kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Dk Slaa, balozi huyo alikiuka sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa kwa kitendo chake ambapo alionekana kupanda kwenye jukwaa la mkutano wa CCM na kuvalishwa kofia ya chama hicho.
Kwa upande wake, Wenje alidai kuwa kwa mujibu wa mkataba wa Vienna Convention wa mwaka 1964 ambao unaeleza mahusiano ya kibalozi unakataza mabalozi kujingiza kwenye mambo ya ndani ya nchi ikiwa pamoja na kushiriki kwenye siasa.
“Mkataba wa Vienna Convention wa mwaka 1964 Ibara ya 41 kifungu kidogo cha kwanza kinakataza mabalozi kujiingiza kwenye mambo ya ndani ya nchi ikiwa pamoja na kufanya siasa.” alisema Wenje na kuongeza;
“Kitendo alicho kifanya balozi wa China kufanya kazi ya uenezi wa chama kimevunja mkataba huo jambo ambalo hatuwezi kulivumilia hata kidogo,”alisema.
Alifafanua kuwa licha ya Ibara hiyo kukataza jambo hilo Ibara ya 3 ya mkataba huo inataja wazi kazi wanazotakiwa kufanya balozi pindi anapokwenda kuwakilisha nchi yake sehemu nyingine.”alisema.
Source: Mwananchi

Monday, September 16, 2013

Dr Mwakyembe Apangua Wajumbe wa Bodi ya Bandari (TPA)

Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amepangua Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanznia (TPA) kwa kusitisha uteuzi wa wajumbe watano wa bodi hiyo. Imeelezwa kuwa wajumbe hao wameondolewa katika nafasi zao ili kuondoa migongano isiyo na tija ndani ya TPA.

Kwa mujibu wa taarifa waliondolewa ni Julius Mamiro, John Ulanga, Caroline Kavishe, Dk Hilderbrand Shayo na Asha Nassoro. Mbali na hao waliondolewa, mjumbe mmoja Dk Jabiri Bakari amejiondoa mwenyewe baada ya ombi lake la kufanya hivo, kukubaliwa Dk Mwakyembe. Waziri amewabakiza wajumbe wawili wa Bodi hiyo ambao ni Said Sauko na Jaffer Machano

Wajumbe wapya ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Kipallo Kisamfu na mwakilishi wa wafanyakazi wa TPA ambaye hakutjwa jina. 

Source; gazeti la Habari Leo​

Padri alitishiwa kifo miezi mitatu kabla!!!

Dar/Zanzibar. Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.

Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Dk Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamili visiwani humo hivi sasa.
“Hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Dk Shein.
Dk Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.
Alisema kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.
“Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na kuongeza:
Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.
“Mara baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi.”
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa 9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet café iliyopo eneo la Mlandege.
Source: Mwananchi

Mr Nice Aingia tena katika mzozo

Dar es Salaam. Nguli wa muziki aina ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda ameingia katika mzozo mzito na meneja wake mpya baada ya kutokukubaliana baadhi ya mambo aliyokuwa akishauriwa na lebo hiyo mpya.

Mr Nice ambaye kwa sasa anamilikiwa na lebo ya Candy&Candy Records  kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa baada ya kutoka katika familia kubwa ya muziki ya GrandPa Recods, ameelezwa kuwa alikuwa na mtazamo tofauti kibiashara na kampuni hiyo hali iliyotishia kuvunjwa kwa mkataba wao.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy&Candy Records, Joe Kariuki alisema kampuni na mwanamuziki huyo anayependwa nchini Kenya ilitokea kutofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.
“Mr Nice ni msanii anayependwa sana hasa Mombasa, lakini wiki chache zilizopita tulikuwa na mabishano kidogo hii ilitokana na mtazamo tofauti hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Akina Mama’ binafsi ule wimbo sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia wimbo mwingine, lakini aling’ang’ania.
“Wimbo ule tuliupiga katika vyombo vya habari kwa bahati mbaya haukufanya vizuri lakini nilimtahadharisha mapema.
“Kampuni inaweza kupata  hasara, lakini tumeamua kuendelea na mkataba kwani kwa sasa ameelewa na tunakwenda kama kampuni inavyotaka,” alisema Kariuki.
Kariuki anasema nyota huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Fagilia’ bado kazi zake zinaendelea kupendwa sehemu mbalimbali nchini humo.
“Tukifika sehemu kama Malindi, Mombasa na maeneo mengine mwanamuziki huyu bado ni chaguo la watu wengi. Anafanya vizuri lakini bado kuna mengi yanayomtinga ila ‘akikaza buti’ hakika atarudi na kuwa kama zamani hata Tanzania atashika chati za juu,” alisema.
Alisema muziki wa Bongo Fleva ni muziki pendwa nchini humo ndiyo maana kampuni hiyo imeingia mkataba na wasanii wengi kutoka nchini Tanzania wakiwamo Four - D, Top C, Mr Nice na Baby Madaha.
Wakati Mr Nice anaingia katika mgogoro huu mpya, miezi michache iliyopita aliondolewa katika Kampuni kubwa ya muziki ya GrandPa Records inayofanya kazi na wasanii wakubwa kama DNA, Ng’ang’a wa Tusker Project Fame na wengine.
Mr. Nice alipigwa chini na kampuni hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshampigisha hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kumwandalia ziara ya kumtambulisha nchi nzima kwa lengo la kumwongezea mashabiki, kumpa shoo ya kumtambulisha na kuachia wimbo mmoja aliofanya na DNA uitwao ‘Tafuta’.
Source: Mwananchi