Blogger Widgets

Thursday, December 11, 2014

BRAND NEW AUDIO: JOH MAKINI FT G.NAKO XO

.
.
Hii ni single mpya ya msanii wa Hip Hop kutokea 87.9 (ArushaCloudsFM)  mwamba wa Kaskazini Joh Makini wimbo unaitwa XO akiwa amemshirikisha G Nako.
Isikilize hapa mtu wa nguvu kisha usisahau kuniandikia ya moyoni ili Joh Makini na G Nako wakipita hapa wasome kutoka kwa watu wao wa nguvu..
Bonyeza hapa kuingia kuisikiliza na kudownload moja kwa moja…. >>>> HAPA
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Monday, December 8, 2014

BRAND NEW VIDEO: G-nako Moralle..

Kutoka Kwa G-Nako WaraWara, hii ndio video yake mpya yaMoralle,, Video imefanyika Arusha, na ni moja kati ya zile Video Tano walizoahidi Weusi.. Kesho, December 9, itakuwepo hewani video ya Joh-Makini I see me.. stay with us..



HII NDIO TWEET YA DAVIDO ILIYOMKOSANISHA NA WATANZANIA..

dvdUsiku wa December 07 Tanzania imechukua tena headline kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hii ni baada ya Mtazania Idris kufanikiwa kushinda kwenye shindano la Big Brother Hot Shot 2014.
Usiku huo huo baada ya ushindi wa Idris,Diamond alipost tuzo aliyoshinda Nigeria baada ya matukio hayo kufanyika,Hit Maker wa single kadhaa ikiwemo Skelewu Davido alipost kitu ambacho kimezua tafsiri tofauti tofauti.
Post ya Davido ilisomeka >>’N they Cheat again lol’ baada ya muda mfupi post hiyo aliifuta ambayo bado Watanzania wamekua na maswali tofauti kuhusu hicho alichokiandika.
1DVD
Post hii ya kejeli, ambayo Davido aliipost kwenye ukurasa wake wa twitter, imemsababishia kujenga uadui na watanzania, na kuambulia matusi yakutosha kwenye social medias hususan kwenye Instagram.

HII NDIO TUZO NYINGINE ALIYOCHUKUA DIAMOND HUKO NIGERIA..

tuzoDiamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine ambayo hizi zilikua zikitolewa Lagos nchini Nigeria ambazo hizi hazikuwa na utaratibu kama wa tuzo zingine kwa kupiga kura.
Baada ya kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kupokelewa na Meneja wake Salaam,Diamond alipost maneno haya>>’Thanks God,we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#samenight Thank you Allah’
Tuzo hizi zinaitwa The Future Awards Prize in Entertainment ambapo kipengele alichokuwa akiwania Diamond alikuwa na wakali mbalimbali akiwemo Panshack au Ice Prince jina lake la zamani wa Nigeria na Michael Kwesi wa Ghana.
dngria

TANZANIA YAKIMBIZA TENA BIG BROTHER AFRICA..

IdrisLeo ni siku ya 63 tangu yaanze mashindano ya Big Brother Africa, ndiyo siku ambayo imefanyika fainali ya #BBAHotshots kwa mwaka huu 2014.
Labda nikukumbushe kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee iliyokuwa imebakiwa na mshiriki wake ndani ya Jumba la BBA katika ukanda wa Afrika Mashariki na tuliona namna ambavyo mastaa wengi wakitoa support kubwa kwa mshiriki huyo ambaye ni Idris.
Hatimaye usiku huu wa Desemba 07 historia nyingine imeandikwa Afrika, ambapo mwakilishi huyo kafanikiwa kuibuka mshindi

Tuesday, December 2, 2014

BRAND NEW AUDIO: Kala Jeremiah ft Nuruwell Usikate tamaa




HAWA NDIO WACHEZAJI WATATU WALIOTAJWA KUWANIA BALLON D'OR

FIFA Ballon d'Or Gala 2012
Orodha ya wachezaji watatu waliongia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Ballon’Dor inayotolewa kwa mchezaji bora wa dunia imetajwa hii leo .
Orodha hiyo imewajumuisha wachezaji watatu ambao ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo  , nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, na Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo  mwaka jana.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo mwaka jana.
Mchezaji ambaye anatetea tuzo hii hadi sasa ni Cristaino Ronaldo ambaye aliitwaa kwa mwaka 2013 na kwa jinsi mambo yanavyokwenda ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo mwakani .
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon'Dor.
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon’Dor.
Mshindi wa tuzo hii atatangazwa kwenye hafla itakayofanyika huko Zurich januari 12 ambapo tuzo mbalimbali zitatolewa .
neur
Kipa wa Ujerumani Manuel Neur atawania tuzo hiyo dhidi ya Lionel Messi na Cristaino

CHEKI PICHA,, HII NDIO AJALI ILIYOMHUSISHA DAVID BECKHAM..!!

becks 2
Moja kati ya story zilizoshtua wapenda michezo nchini England mwishoni mwa wiki hii ni ajali ambayo aliipata nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England David Beckham .
Becks alipata mkasa huo wakati akiwa anatoka kumchukua mwanae anayefahamika kwa jina la Brooklyn toka kwenye mazoezi ya kila siku ya timu yake ya Arsenal .
Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Gari ya Beckham aina ya Audi iligongana na gari nyingine ndogo na star huyo alipata jeraha kwenye bega lake japo halikuwa jeraha kubwa sana .
Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Mtoto wa star huyo Brooklyn amabye ni mchezaji wa timu ya Vijana ya Arsenal hakuumia kwenye ajali hiyo ambayo magari yote yaliyohusika yaliharibika vibaya .
Picha inayoonyesha familia nzima ya Beckham akiwa na mkewe Victoria Beckham na wanae wa kiume Brooklyn , Romeo na Cruz.
Picha inayoonyesha familia nzima ya Beckham akiwa na mkewe Victoria Beckham na wanae wa kiume Brooklyn , Romeo na Cruz.

Thursday, November 13, 2014

BREAKING NEWS: Msanii wa HipHop Geez Mabovu afariki Dunia..

Geez Mabovu
Geez Mabovu ni ambae hajavaa shati.
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2

Friday, November 7, 2014

MPYA HII KUTOKA WHATSAPP,, WAONGO SASA BAASI..

whatsapp-doble-checkNakumbuka moja ya taarifa kubwa zilizowahi kuchukua headlines mwezi Februari 2014 ilikuwa ni stori ya kuuzwa kwa mtandao wa Whatsapp kwa mmiliki wa Facebook, leo kuna taarifa nyingine mpya kuhusiana na watumiaji wa mtandao wa Watsapp.
Haya ni mambo manne mapya ambayo huenda hujayasikia kuhusu WhatsApp;-
1. Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
2. Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
3. Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
4. Ukibonyeza ujumbe uliotuma utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
whatsapp
Kuanzia jana huduma hiyo itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Ukibonyeza ujumbe wenyewe itakuonyesha muda ambao uliyemtumia ujumbe huo kausoma.
Tazama video hii uone mabadiliko hayo.

BRAND NEW: HII NDIO TRACK YA GOSBY INAYOITWA "WEMA SEPETU" ILIYO MAKE HEADLINES..

Gosby
Kila alieona jina la wimbo ‘Wema Sepetu’ amekua na hamu ya kujua moja kwa moja nini kimeimbwa ndani ya hii single ya mkali Gosby ambayo single zake zilizotangulia kama ile ya ‘Monifere’ ft. Vanessa Mdee zimempa nafasi ya kupokewa zaidi na Wabongo.
Ukitaka kuisikiliza na kudownload hii mpya ya ‘Wema Sepetu’ unaweza kubonyeza hapa

DOWNLOAD 

Saturday, November 1, 2014

HAYA NDIYO ALIYOSEMA CHID BENZ KUHUSIANA NA YE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AIRPORT..

Screen Shot 2014-11-01 at 3.14.15 AMImekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.
Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
Screen Shot 2014-11-01 at 3.14.00 AMKuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>> ‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake… tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji, tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’
Screen Shot 2014-11-01 at 3.39.11 AMKuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’
Screen Shot 2014-11-01 at 3.44.09 AM‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.

Friday, October 24, 2014

UMESIKIA HII YA BOKO HARAM KUTEKA WANAWAKE WENGINE? HEBU CHEKI NAYO HAPA..

Nigeria Kidnapped GirlsTaarifa iliyoripotiwa na shirika la utangazaji Uingereza BBC imesema kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram kimefanya mashambulizi katika kijiji cha Adamawa kilichopo Kaskazini Magharibi ya Nigeria na kuteka wanawake na wasichana katika kijiji hicho.
Utekaji wa wasichana na wanawake hao unatokea ndani ya siku sita tangu serikali ya Nigeria na kikundi hicho walipofanya makubaliano ambapo Boko Haram waliahidi kuwaachilia huru zaidi ya wasichana 200 wanaoshikiliwa na kikundi hicho.
Japo Boko Haram wamekiuka makubaliano waliyoafikiana Ijumaa iliyopita, bado serikali ya Nigeria ina matumaini ya kuachiliwa huru kwa wasichana hao baada ya kikao kinachotarajiwa kufanyika muda wowote kuanzia sasa huko Chad.

BRAND NEW: UMEISIKIA HII COLABO YA FA NA ALI KIBA? PITA NAYO HAPA..!

MwanaFAMwanaFA ambae hivi karibuni alitajwa na producer maarufu Hermy B kama Mkali miongoni mwa wachache bongoflevani wenye uwezo mkubwa wa kuandika pia mashairi, ameungana na Ali Kiba kuziteka headlines za bongofleva kwa single yao ambayo unaweza kuipakua hapa kupitia mkito.com

Wimbo ni wa mwana FA akiwa amemshirikisha Ali Kiba, na unaitwa Kiboko Yangu..
mkito.com ni tovuti mpya iliyo chini ya vijana walioamua kuwa serious kuongeza vipato vya Wasanii wa Tanzania hivyo kila unaposupport kwa kudownload au kusikiliza hii single ndivyo unaongeza kipato cha wakali hawa.
Au unaweza kuibonyeza hapa kupelekwa moja kwa moja kuipata >>> HAPA

UMEIPATA HII YA CHID BENZ KUKAMATWA NA POLISI AIRPORT? ICHEKI HAPA..

Najua kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid Benz amekamatwa na Polisi.
Taarifa zinasema kakamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Mbeya na hiyo imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni kosa kwa yeyote kukutwa navyo.
Wakati millardayo.com inaendelea kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi, tumezungumza na muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz ndio alikua anakwenda kushiriki kesho.
Chidi 1Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu >>> “Sijapewa taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba haviruhusiwi kupita Airport
Chidi Benz alikua ameongozana na msanii mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi kabaki na Polisi na Shetta amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea Mbeya.

Monday, October 20, 2014

HAYA NDIO DIAMOND NA UONGOZI WAKE WALIYOZUNGUMZA BAADA YA FIESTA KUWAENDEA VIBAYA..!!

dmnOctober 18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Ilikua ni good time ya ukweli sana Watanzania kumuona T.I kumuona Davido kumuona Victoria Kimani na Waje pamoja na wasanii wengine wa kimataifa ambao nao walihudhuria tamasha hili lililokuwa na watazamaji zaidi ya elfu hamsini.
Miongoni mwa wasanii waliopokelewa vizuri kwenye show hii ni pamoja na Mr Blue na Micharazo,Ally Kiba,Weusi,Vanessa Mdee,Stamina pamoja na Diamond Platnumz ambaye aliimba single 4 kwenye jukwaa hili.
Mashabiki wengi wa Ally Kiba inasemekana walipanga kuzomea wakati Diamond Platnumz anaperfoam pale jukwaani,kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm meneja wa Diamond Platnumz aitwae Babu Tale kaongelea hali hii.
taleHizi ni sentensi 10 alizozisema.
1.Sisi tumechukulia  sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura Diamond kwenye tuzo za Channel  O Music Awards, kwa sababu mwisho wa siku chema chajiuza kibaya chajitembeza.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Sunday, October 12, 2014

UMESIKIA KUHUSU HII FILAMU YA MAISHA YA LIONEL MESSI? Cheki Trailer ya Movie hiyo hapa..!!


Labda unapokuwa mtu maarufu duniani, unahitaji filamu itakayokuelezea maisha yako halisi, Lionel Messi kama mchezaji bora wa soka Duniani amefanikiwa kupata bahati hii ya kutengenezewa filamu.
Filamu hiyo iliyoongozwa na director Alex De La Iglesia, pamoja na kuhusisha maisha ya Messi pia imewahusisha marafiki na wanasoka wenzie Messi, kama vile Pep Guardiola, Pique, Pinto, Iniesta, na Mascherano, pia wachezaji wenzie wa timu ya Newell’s Old Boys.
Pamoja na kutokuwepo kwa Messi mwenyewe halisi, muongozaji filamu, Alex de le Iglasia amefanikiwa kuonyesha picha halisi ya maisha ya nahodha huyo wa Argentina.
Filamu hiyo ilizinduliwa jijini Rio de Janeiro na sasa inaonyeshwa kwenye kumbi za sinema huko Amerika ya kusini.
Tazama trailer ya Movie hiyo hapa..

Saturday, October 11, 2014

BRAND NEW: Ile Video ya Umebadilika kutoka kwa Young Killer na Banana Zoro si ndio hii hapa sasa..

Young Killer 67Kwenye mfululizo wa single zake alizowahi kutoa hii ni ya 5 ikiwa ni baada ya Dear Gambe,Jana na Leo,Mrs. SuperStar,My Power na hii inaitwa Umebadilika ambapo mwanzoni ilifanywa Classic Sound lakini ikaja kurudiwa na Combination Sound kwa Man Water.
Video imefanywa na Director Hefemi Mtanzania ambae anaishi na kufanya kazi nchini Marekani.

Thursday, October 9, 2014

BRAND NEW VIDEO: HIVI NDIVYO NAKAAYA ALIVYORUDI KWENYE GAME

Screen Shot 2014-10-09 at 10.37.45 AMNakaaya ni staa wa bongofleva ambae ujazo wa jina lake ulitokana na ‘Mr. Politician‘ ambapo baada ya hapo aliendeleza harakati zake kwenye huu muziki mpaka alipopata ajali Arusha ambayo ilimfanya awe kimya kwa muda mrefu.
Nakaaya ambae pia ni mama wa mtoto mmoja alietimiza mwaka mmoja siku chache zilizopita alirudi kwenye muziki baada ya kujifungua na kutoa single ya kwanza iitwayo ‘blessing‘ ambayo ni dedication pia kwa mwanae.
VIDEO IMEFANYWA NA CYNE STUDIOS ARUSHA.. Itazame hapa..


Wednesday, October 8, 2014

HII NDIO SABABU YA RAIS WA ZANZIBAR KUMFUKUZA KAZI MWANASHERIA MKUU, OTHMAN M. OTHMAN..!!

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amemfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. OTHMAN MASOUD OTHMAN kwa kuvikataa baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba.

Nini maoni yako kuhusu hili?

Photo: Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amemfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. OTHMAN MASOUD OTHMAN kwa kuvikataa baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba.

Nini maoni yako kuhusu hili?

Thursday, September 25, 2014

Msikilize hapa T.I na alichokisema kuhusu kuja Bongo..!

T.I 3Kupitia XXL ya CloudsFM September 23 2014 ndio T.I ametangazwa kuwa staa wa muziki wa kimataifa ambae atakua mgeni kwenye stage ya Fiesta 2014 Leaders Club KinondoniOctober 18.
T.I ni rapper kutokea Atlanta Georgia Marekani na umri wake ni miaka 33 na ni mkali wa hiphop duniani ambae ujazo wa jina lake ulianza kuonekana mwaka 2003 pale aliposhirikishwa na Bone Crusher kwenye single ya ‘never scared
T.I 2

Huu ndio Mchongo alioupata Diamond Kwenye App Mpya ya "Mziiki"

Diamond PlatinumzIngawa hajaweka wazi namna dili hii itakavyokuwa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram,Diamond Platnumz amepost picha ambayo imebeba maandishi yasemayo ‘Ningependa kukutaarifu shabiki wangu pendwa kuwa kijana wako sasa ni balozi wa application mpya iitwayo Mziiki’.
Hii ni application ambayo itatumiwa na watu wenye simu za androad kusikiliza muziki huu ndiyo muonekano wake utakapokuwa ume instal kwenye simu yako.
mond3
Maandishi ya Diamond pamoja na alichokipost ni hiki.
mond
mond 2

Monday, September 15, 2014

BRAND NEW: KUTOKA KWA PROFFESOR JAY, HIZI NDIO VIDEO MBILI ALIZOZIACHIA KWA PAMOJA..!


Rapper mkongwe  Joseph Haule aka Professor Jay usiku wa Jumamosi (13 Sept) alizindua video mbili ‘Kipi Sijasikia &  ‘3 Chafu’,uzinduzi huo ulifanyika ndani ya ukumbi wa Ten Lounge uliopo maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam
Mbali na uzinduzi huo Professor alipata support kutoka kwa wasanii mbalimbali  akiwemo,Linex,Chid Benz,Lady Jay Dee,Soggy Doggy,TID,Slim,D Knob,Country Boy na wengineo..
Video zenyewe ndio hizi hapa, zitazame na utoe maoni yako..



Na video ya pili ni hii ya Tatu chafu.. itazame hapa..

Wednesday, September 10, 2014

ULIONA HII? HIZI NDIO PRODUCTS MPYA KUTOKA APPLE

news newsNajua kuna uwezekano ukawa ulisikia fununu sana kuhusu iPhone6 au hata kuona baadhi ya taarifa feki kuhusu simu hii mpya, post hii ni maalum kukuletea taarifa sahihi na ya ukweli kuhusu iPhone6 ambayo ndio imetambulishwa rasmi.
Wanasema simu zote hizi mbili mpya zina A8 processor ambayo inafanya ziwe na kasi zaidi kuliko iPhone5 kwa asilimia 20.
iphone 6 1
Unaambiwa zote iPhone6 na iPhone6 plus zimekuja na screen kubwa tofauti na nyingine zilizotangulia
iphone 6 2
Apple wenyewe wanasema simu hizi mbili za iPhone6 na iPhone 6 plus zina 8 megapixel camera ambayo itasaidia camera kupata focus faster.
iphone 6 3
Simu hizi zote mbili zitaanza kupatikana nchini Marekani September 19 2014 nchini Marekani pamoja na kwenye nchi nyingine nane duniani.
iphone 6 4
Simu hizi za iPhone 6 na iPhone 6 pluz zitaambatana na saa hii ambayo unaweza kuitumia kufanya mambo mbalimbali ambayo yapo kwenye simu pia
iphone 6 5
Apple wanasema malengo yao ni k’uireplace’ au kuichukua nafasi ya Wallet, yani kurahisisha mambo kwenye iPhone kiasi kwamba hutohitaji kutembea na wallet.
Mengine yaliyosemwa ni pamoja na >>  ‘the bigger displays allow for bigger batteries: 11 hours of video watching on the iPhone 6 and 14 hours for the iPhone 6 Plus — up from 10 hours on the iPhone 5S
And the iPhones will come with Apple’s new iOS 8 software, featuring a new HealthKit application that monitors users’ heart rates, sleep, weight and blood pressure among other health-related information. Apple said iOS 8 will be available Sept. 17 to customers who have an iPhone 4S, iPhone 5, iPhone 5C or iPhone 5S.
iphone 6
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.