
Mchezaji wa Barcelona, Dani Alves, juzi alitoa kali ya mwaka baada ya kula ndizi aliyotupiwa na washabiki wa timu pinzani kama ishara ya ubaguzi wa rangi.. Tukio lilitokea juzi jumapili katika mchezo baina ya club ya Barcelona na Villareal.
Mchezaji huyo Raia wa Brazil alikuwa tayari kupiga kona mara ghafla ndizi iliyorushwa kutoka kwa washabiki ilitua mbele yake na kwa ujasiri aliokota ndizi hiyo, akaimenya na kuila kisha akapiga kona iliyozaa...