Hotuba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, imepondwa vikali na wasomi mbalimbali wasiofungamana na upande wowote kisiasa.
Juzi Dk. Slaa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kufuatia kujiweka kando kujishughulisha na Chadema kutokana na na chama hicho kumpokea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kumpitisha kugombea nafasi ya urais akiviwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ajitokeza hadharani na kutoa msimamo wake wa kustaafu siasa, huku akimtuhumu mgombea huyo...