Blogger Widgets

Friday, February 7, 2014

FBI inayo miili ya magaidi wa Westgate..!!!


Mmoja wa magaidi walioshambulia Westgate
Mkuu wa majeshi ya Kenya ameabia vyombo vya habari kuwa shirika la Ujasusi la Marekani FBI lilikabidhiwa miili ya magaidi walioshambulia jengo la Westgate nchini Kenya mwaka jana.
Karangi, ameyasema hayoalipokuwa akikitoa maelezo katika mkutano ulioandaliwa nchini Kenya na baraza la vyombo vya habari kuhusu ambavyo shambulizi hilo lilishughulikiwa.
Alisema kuwa majeshi yake hatimaye yaliweza kuwaua magaidi hao, siku mbili baada ya kuvamia Westgate tarehe 21 mwezi Septemba 2013.
Magaidi hao walifyatua risasi kiholela na kuwaua takriban watu 67 huku mamia ya wengine wakijeruhiwa.
Bwana Karangi aliongeza kwamba baada ya shambulizi kuanza Jumamosi magaidi waliuawa siku iliyofuata.
''Miili ya magaidi hao ilikabidhiwa majasusi wa FBI,'' alisema Karangi ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Washambuliaji wote wanne walikuwa wenye asili ya kisomali ingawa mmoja kati yao alikuwa ameishi zaidi nchini Norway
Maafisa wa usalama wakati huo wakipambana na magaidi hao walikuwa wametoa taarifa kuwa Westgate ilivamiwa na ilivamiwa na magaidi 12 ingawa idadi yao baadaye ilisemekana kuwa magaidi wanne pekee
Wanamgambo wa Somalia Al- Shabaab walidai kutekeleza mashambulizi hayo wakisema kuwa ilikuwa onyo kwa serikali ya Kenya kukoma kujihusisha na vita nchini Somalia ambako wanasadia majeshi ya Muungano wa Afrika kupambana dhidi ya Al Shabaab.

Lady Jay Dee seeks divorce from husband...!!!





Posted  Friday, February 7  2014 at  14:54
IN SUMMARY
  • According to recent reports that have since been circulating and confirmed by Gadner himself, the talented musician and owner of the famous Nyumbani Lounge threatened for a divorce after learning that her husband had secured a deal of becoming a radio presenter in Kenya, a deal that will see him cash in Sh 6million a month.
Dar es Salaam. Word has it that Lady Jay Dee is seeking a divorce from her husband and manager, Gadner G Habash.
According to recent reports that have since been circulating and confirmed by Gadner himself, the talented musician and owner of the famous Nyumbani Lounge threatened for a divorce after learning that her husband had secured a deal of becoming a radio presenter in Kenya, a deal that will see him cash in Sh 6million a month. Those close to the couple claim that Jay Dee can’t just stand seeing her husband cross over to Kenya, when he is her manager.
“You need to know that all Jay Dee’s projects are being overseen by Gadner, she knows very well that if she lets him go, they will all collapse and that is why she threatened for a divorce,” claimed the source.
Gadner has since reversed his decision following the threats of putting their nine year marriage to an end.
Source: The Citizen

Facebook yagonga miaka 10..!!!

Facebook inasherehekea miaka kumi wiki hii tangu kuzinduliwa. Ina watumiaji bilioni 1.2. Lakini nani anatumia Facebook na wanaitumia kwa njia gani?

Mishumaa kwenye keki ya Facebook inaposherehekea miaka 10 haitazima kabla ya mtu kuwa na tashwishi ikiwa kampuni hiyo itadumu na kufikisha mwaka wake wa 11.
Wakuu wa Facebook wakisherehekea miaka 10
Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, ikiwa utaaminika , siku za mwisho za Facebook zinakaribia.
Taarifa mbali mbali zinapendekeza kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa Facebook, vijana wakiwemo wengi, wanachoshwa na mtandao huo wa kijamii baadhi ya watafiti wakisema kuwa watumiaji wengi wanalinganisha Facebook na maradhi mabaya.
Utafiti kama huu ambao huambatanishwa na picha ya Mark Zuckerberg mwasisi wa mtandao huo akionekana mwenye huzuni huonyeshwa sana na vyombo vya habari na hata kusambazwa zaidi kwenye Facebook.
Kwa hivyo wakati watafiti waliposema kuwa kampuni hiyo itapoteza asilimia themanini ya watumiaji wake katika kipindi cha miaka mitatu, wakuu wake walijibu kwa ukali.
Facebook ina watumiaji wengi zaidi vijana kuliko mtandao mwingine wowote.
Imekuwa ikibadili sura yake tangu mwaka 2004.
Mark Zuckerberg
Hata hivyo baadhi ya watafiti wanasema kuwa karibu vijana milioni tatu waliondoka kwenye Facebook katika miaka mitatu iliyopita nchini Marekani.
Vijana wengi wanasema waliacha kutumia Facebook kwa sababu ya wazazi wao, ambao pia wamejiunga na mtandao huo wa kijamii.
Wazazi hutuma picha za watoto wao kwenye mtandao ambazo wao wenyewe wanahisi ni za kuchekesha.Jambo hili limewatia aibu vijana ambao wameamua kutumia mitandao kama WhatsApp au Snapchat badala ya kuwa kwenye mtandao mmoja na wazazi wao.
Licha ya vijana wanaotumia Facebook kupungua watu wenye umri zaidi ya 55 wameonekana kuongezeka.

Sasa je ni hali ya vijana kuondoka Facebook na kuwachia watu wazima nafasi kutumia mtandao huo? Je utafikisha miaka 11? Wataalamu wana shaka na hilo. Wewe je? Bado utahitaji Facebook mwaka ujao?
Source: BBC