Blogger Widgets

Saturday, April 18, 2015

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA YALIYOJIRI KATIKA ONESHO LA MISS AND MR.IAA JANA IJUMAA..

Kutoka katika ukumbi wa Club D Arusha, hizi ni baadhi picha za onesho la Kumtafuta Miss na Mr. wa chuo cha uhasibu Arusha. Hii ilifanyika jana Ijumaa, kwenye ukumbi wa juu wa club D moshono..
Mshindi Wa Mr.IAA 2015

Chief Judge, Idris Sultan akitangaza washindi

Washindi wa Miss and Mr.IAA 2015

Mshindi wa Miss IAA 2015



Former Miss IAA 2014

Majudge wa shindano hilo..

Washiriki wa Miss IAA 2015

Mshiriki wa Mr.IAA 2015

Mshiriki wa Mr.IAA 2015

Red Carpet

Red Carpet
Msanii G.Nako kutoka kundi la weusi akiperform katika shindano hilo


Msanii Hisia, akiperform katika shindano hilo..

PICHA ZOTE KWA HISANI YA CLIQUE PIXELS ARUSHA

Friday, April 10, 2015

UMESIKIA HABARI HIZI KUHUSU MTANZANIA ANAYEHUSISHWA NA TUKIO LA UGAIDI KENYA??


Mtanzania aliyekamatwa Kenya akidaiwa kufanya ugaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa uliosababisha vifo vya watu 148, Rashid Charles Mberesero (20) ni mwanafunzi wa kidato cha tano, lakini uongozi wa shule anayosoma umesema alitoweka shuleni hapo Desemba Novemba 2014.
 
Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.
 
Mama mzazi wa kijana huyo, Fatuma Ali alisema jana kuwa: “Baada ya kufaulu alichaguliwa kujiunga na Sekondari ya Bihawana na likizo alirudi nyumbani na baada ya likizo kuisha aliniaga anarudi shuleni.”
 
Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi.
 
Mwendesha mashtaka, Daniel Karuri alisema, “Rehani Dida” hakufikishwa kortini kwani alikuwa na wapelelezi mjini Garissa kukusanya ushahidi zaidi, baada ya kukiri kuwa ni mfuasi wa kundi la Al-Shabaab.
 
Mtanzania huyo anadaiwa kukamatwa baada ya kujificha kwa saa nane akiwa amejichanganya na maiti, lakini baadaye alipanda na kujificha darini akiwa na mabomu.
 
Kauli ya wazazi
Jana, mama huyo, aliwaambia  waandishi wa habari kuwa haelewi ni nani aliyemshawishi mwanaye kujiunga na kundi hilo na kwamba jambo hilo limemshtua.
 
“Hizi taarifa tumezisikia na kuona kwenye TV na kwa kweli zimetushtua sana, mimi nahisi huko shule ndiko alikokutana na watu wabaya,”alisema Fatuma ambaye ni mkazi wa Gonja wilayani Same.
 
Baba mzazi wa mtuhumiwa huyo, Charles Mberesero Temba, alikiri kuwa Rashid ni mtoto wake ambaye alizaa na Fatuma mwaka 1994 na miaka yote alikuwa akiishi na mama yake.
 
“Huyo mtoto sijawahi kuishi naye, muda wote tangu 1994 alikuwa akilelewa na mama yake,” alisema Temba na kuongeza kuwa hakuwahi kuishi na mzazi mwenzake huyo.
 
“Mwaka jana mama yake ndipo alinikutanisha na mtoto na akanitambulisha na mimi nikamshauri abadili dini kwa sababu mimi ni Mkristo Mkatoliki,” alisema.
 
Alisema aliendelea kuwasiliana naye na aliwahi kumpeleka kanisani mara tatu akimshauri abadili dini ili arudi kwenye dini ya baba, lakini alikataa.
 
Alisema inavyoonekana ushauri wake huo haukupokewa vizuri na mwanaye na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mawasiliano baina yao kukatika.
 
Kutoka Bihawana
Habari zilizopatikana jana kutoka shuleni Bihawana zilisema kuwa Mberesero alitoroka shuleni Novemba mwaka jana, baada ya kukaidi kuvua kofia katika eneo la shule.
 
Mkuu wa Shule hiyo, Joseph Mbilinyi alisema alimpokea mwanafunzi huyo Agosti 15, mwaka jana akitokea katika Shule ya Sekondari ya Kigwe wilayani Bahi.
 
Alisema mwanafunzi huyo alipata uhamisho baada ya kubadilisha masomo kutoka masomo ya sanaa mchepuo wa Historia, Jiografia na Kiswahili (HGK) na kuingia katika masomo ya sayansi ya Fizikia, Kemia na Biolojia (PCB).
 
Mbilinyi alisema katika shule hiyo wanafunzi walikuwa na mazoea ya kuvaa rozali na kofia, jambo ambalo alilipiga marufuku lakini Novemba 24, mwaka jana alikutana na kijana huyo akiwa amevaa kofia.
 
“Nilimwambia aivue aichanechane mbele yangu, lakini alikataa na kunijibu kuwa amezoea kuivaa na hawezi kuichana. 
  
"Kwa sababu ilikuwa ni usiku niliondoka na kofia hiyo na kumwambia kesho yake asubuhi aje ofisi kwangu ili tumalize suala hilo, alikuwa ni mtu wa kwanza kufika ofisi kwangu. 
  
"Nilimwambia anieleze kwa nini hataki kuichana, ningeweza kumsaidia kumtafutia shule ambazo zinaruhusu mavazi hayo.”
 
Alisema hata baada ya mazungumzo hayo, Rashid hakueleza kwa nini alikataa kuichana ndipo alipoambiwa kuwa angerejeshwa nyumbani ili aje na mzazi wake na aichane mbele yake.
 
“Kwa kawaida wanafunzi wengine ukiwaeleza hivyo, huwa wanaomba msamaha yanaisha lakini kwa Rashid ilikuwa ni tofauti, aliniambia yuko tayari kurudishwa nyumbani lakini siyo kuchana kofia hiyo,” alisema.
 
Mwalimu huyo aliongeza: “Niliona njia ya kumsaidia ni kuwashirikisha walimu ambao wanasimamia msikiti wetu huu. Walimu walimuita na akakubali kupewa adhabu ili jambo hilo liishe bila kufikishwa kwa wazazi wake.”
 
Hata hivyo, alisema baada ya mazungumzo hayo, Rashid alichukua begi lake na kuondoka kwenda mjini na kuwaacha wenzake wakimalizia mtihani wa Biolojia.
 
“Nilipata shida sana sikupenda mwanafunzi huyu aondoke shuleni, nilitaka hili jambo lipate suluhu. Nilipigia simu alizoandikisha shule ikiwamo ya baba yake bila mafanikio kwa sababu hazikupokewa, isipokuwa moja ambayo ilipokelewa na mwanamke ambaye alikana kumfahamu.
 
“Hadi leo bado ni mwanafunzi wetu kwa sababu kanuni zinasema baada ya siku 90 kama mwanafunzi hajaonekana shuleni, tunapeleka jina kwenye Bodi ya Shule ambayo itatoa uamuzi,” alisema.
 
Katibu mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu katika shule hiyo, Mungi Ramadhan Mungi alisema Rashid alikuwa ni mtu wa msimamo, akitaka jambo lake hata kama halina usahihi analisimamia.
 
“Aliwahi kutaka kupigana msikitini mara mbili, mara ya kwanza tulikuwa tukiuliza maswali kuhusu masomo ya darasani yeye akasema hairuhusiwi kufanya hivyo msikitini,” alisema.
 
Alisema hatua hiyo ilizua mabishano na alifikia uamuzi wa kutaka kuwachapa walioongelea mambo ya masomo ndani ya msikitini.
 
“Alikuwa ni mtu wa msikitini na bwenini mara nyingi hakupenda kuchanganyika na wenzake, jambo hilo lilimfanya hata kukosa marafiki,”alisema.
 
Alisema aliwahi kuwahadithia kuwa alibadili dini akiwa anasoma sekondari huko Moshi.
 
Mwalimu anayewasimamia wanafunzi wa Kiislamu, Mohamed Mwijuma alisema baada ya Rashid kutoroka shuleni hapo waligundua alikuwa ni mwanafunzi aliyekuwa na matumizi yasiyo ya kawaida.
 
“Pia tuligundua kila mwisho wa wiki alikuwa akitoroka kwenda mjini,”alisema Mwijuma ambaye alishiriki kulipatia ufumbuzi tatizo hilo la kukutwa na kofia shuleni.
 
Hata hivyo, alisema Februari mwaka huu, Rashid alirejea mwisho wa wiki na kuondoka moja kwa moja na mizigo yake yote.
 
Habari zilizopatikana shuleni hapo zilisema baada ya Rashid kutajwa kuhusika na tukio hilo, mama yake mzazi alifika shuleni hapo kumtafuta mwanaye.

Thursday, April 9, 2015

HII NDIO AJALI MBAYA ILIYOTOKEA TANGA LEO..

IMG-20150409-WA0018
Ajali nyingine tena imetokea Tanga leo APRIL 9 2015, taarifa za awali zinasema watu 10 wamefariki na wengine wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni Tanga, gari zilizopata ajali hiyo ni basi la NGORIKA, jingine la RATCO pamoja na gari nyingine ndogo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, RPC Juma Ndaki kathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba mwendo kasi umechangia kutokea ajali hiyo.
Hizi ni PICHAZ ambazo zimeenea mitandaoni zikionesha jinsi hali ilivyo eneo la tukio.
IMG-20150409-WA0014IMG-20150409-WA0015
IMG-20150409-WA0016
IMG-20150409-WA0017
IMG-20150409-WA0018
IMG-20150409-WA0013

Saturday, April 4, 2015

Ulikuwa unajua sababu ya Charles Hilary kuondoka BBC? Hii ndio sababu..

 Chaz 1
Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata kupitia Radio One pia.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alithibitisha Hillary kutarajiwa kujiunga na Azam Media akiwa na historia nzuri kwenye vyombo vya habari kuanzia alipoanza mwaka 1994 Radio one na kabla ya hapo alitokea radio Deutsch Welle na mwaka 2006 alijiunga na BBC.

Ulisikia Kuhusu Reginald Mengi kufunga Ndoa na K-Lyn? Cheki picha Hapa..

Germany France Plane CrashMtandao wa Bongo5.com umepata nafasi ya kupokea pichaz Exclusive kutoka kwenye harusi hii ambayo imefungwa kwenye ardhi ya nchi ya Mauritius kwenye mwisho wa mwezi March 2015.
Hii ndoa pia ilishuhudiwa na watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.
Germany France Plane CrashNdoa imefungwa miezi minne baada ya Reginald Mengi kumchumbia Jacky Dubai kwenye siku ya kuzaliwa ya mrembo huyu December 2014.
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash
Germany France Plane Crash

Ulisikia hii ya Ajali ya mashabiki wa Simba Ukawa? Chanzo ni hiki hapa..

AJALI DOMHii ilianza kuchukua Headlines jana April 03 kuhusu ishu ya ajali ambayo walipata mashabiki wa Timu ya Simba waliokuwa wakisafiri kwenda Shinyanga kushabikia Timu yao ambayo itakuwa ikipambana na Kagera Sugar leo April 4.
Leo imetawala pia katika vyombo vya Habari, Ripota wa Clouds FM Morogoro aliripoti tukio hilo, amesema ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya Morogoro ambapo mvua inaendelea kunyesha, utelezi wa Barabarani ukafanya gari hiyo kupata ajali.
Watu saba wamefariki na wengine 18 ni majeruhi ambao walipelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.