Blogger Widgets

Friday, April 26, 2013

MBUNGE WA ARUSHA MJINI AVAMIWA NA POLISI NA KUKAMATWA USIKU WA MANANE NYUMBANI KWAKE!!!

Godbless Lema alipowasili chuo cha Uhasibu Arusha


 Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, ametiwa hatiani na jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi wa vurugu zilizojitokeza siku ya jumatano katika chuo cha uhasibu Arusha. Pia imedaiwa kuwa mbunge huyo ndiye aliyesababisha wanafunzi wa chuo hicho wamfanyie vurugu mkuu wa mkoa wa Arusha alipofika katika eneo hilo. Usiku wa kuamkia Leo, Polisi wamevamia nyumba ya Mbunge huyo... Read More >>>

Wednesday, April 24, 2013

Habari kamili na picha juu ya tukio la mgomo wa Wanafunzi Chuo cha Uhasibu Arusha..

Reported by Aloyce Jerry

Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka kuyawasilisha wenyewe. Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi, Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao. "Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema Mheshimiwa Lema.
Mh.Godbless Lema akihutubia wanafunzi waliokusanyika eneo la "freedom square" chuoni hapo.

Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi hao, akidai kwamba hawezi kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda kuzungumza na pia alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake kuzungumza na watu wasio na nidhamu. Maneno hayo yalipandisha hasira ya wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti kikaandaliwa katika ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili mkuu huyo azungumze.

Wanafunzi walikusanyika eneo hilo kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea, wanafunzi walisikika wakimzomea kwa madai kwamba ameonesha dharau. Wanafunzi walianza kuzomea na kumrushia chupa zaa maji mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi mabomu ya machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho. Kwa muda wa masaa mawili imekuwa ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo mpaka hali ilipo tulia kabisa.

Kwa sasa hali ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi. Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio


Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha

MABOMU YA MACHOZI NA RISASI ZATUMIKA KUWATULIZA WANAFUNZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA!!!!

Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha chalazimika kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wametanda chuoni hapo na kugoma kumsikiliza mkuu wa mkoa, kwa madai kwamba ana dharau. Mabomu na risasi zilirindima eneo hilo huku wanafunzi wakikimbia hovyo huku na kule kwa hofu na woga. Picha na habari zaidi zitakujia hapa hapa...

MKUU WA MKOA AGOMA KUONGEA NA WANAFUNZI KWA MADAI HAWEZI KUONGEA BILA KIPAZA SAUTI!!!

Baada ya mkuu wa mkoa kufika chuo cha uhasibu Arusha,
alishindwa kuongea na wanafunzi hao kwa madai kwamba hawez kuzungumza bila kipaza sauti.

"Mkuu wa mkoa mwenyewe anaitwa hapa kwenye tukio anakuja kama anakuja kwenye send-off wakati kaitiwa msiba hapa" Ni maneno ya mbunge wa jimbo la Arusha bwana Godbless Lema.. pia Lema amesikika akisema "Mkuu huyo wa mkoa amekuja hapa si kwa ridhaa yake, bali ni cheo tu kimemleta hapa" Wanafunzi wa chuo hicho kwa sasa hawataki kusikia lolote ni maandamano tu wanatka. HABARI ZAIDI UTAZIPATA KUPITIA HAPAHAPA...





BREAKING NEWS!!!!! YANAYOJIRI NOW CHUO CHA UHASIBU ARUSHA!!!

Wanafunzi wagomea masomo na kudhamiria kuandamana kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kisu usiku wa jana, saa nne usiku wakati akitokea chuo kujisomea. Katika picha ni matukio yanayoendelea sasa chuoni hapo, wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha bwana Godbless Lema.. 




KINACHOENDELEA NOW KATIKA PICHA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA...