Blogger Widgets

Wednesday, October 23, 2013

SHULE ZA SEKONDARI NCHINI KUUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO..!!

0002_1ab10.jpg
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ukianzia Shule ya Kambangwa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Meneja wa Samsung Tanzania Kishor Kumar, wapili ni Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom, Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng'wigulu.
0003_8d170.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung. Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng'wigulu, na Mtaalamu wa komputa wa Samsung, Julius Giabe.
0004_05253.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame, akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo wa taifa wa mawasiliano, uliofanyika kwa kuanzia na shule ya Msingi Kambangwa ya jijini Dar es Salaam.
0005_d4b71.jpg
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung. Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, na Mtaalamu wa komputa wa Samsung, Julius Giabe.
0006_217d7.jpg
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kambangwa, wakitoa burudani kwa wageni waalikwa, Wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari na Mkongo na Taifa wa Mawasiliano.(P.T)

Serikali yafikiria kuondoa kodi ya ving’amuzi..!!

Arusha. Serikali inakusudia kupunguza au kuondoa kabisa kodi katika ving’amuzi ili kuwezesha Watanzania wengi kumudu kununua vifaa hivyo na kupata huduma ya matangazo ya runinga.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa kwa sababu Serikali inatekeleza makubaliano ya kimataifa ya kuhamia mfumo wa dijitali kutoka analojia, ni vyema kila Mtanzania akawa na uhakika wa kupata huduma ya matangazo ya runinga na hilo haliwezi kufanikiwa iwapo bei ya ving’amuzi itaendelea kuwa juu.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba PICHA|MAKTABA 


Akizungumza kwenye mkutano wa 21 wa Umoja wa Taasisi za Utangazaji Kusini mwa Afrika (Saba), Makamba alisema hivi sasa wizara yake inawasiliana na Wizara ya Fedha pamoja na wadau wengine kuangalia njia bora na sahihi ya kufanikisha lengo hilo.
“Tayari serikali imepunguza viwango vya kodi kwenye ving’amuzi ili kuwapa nafuu wananchi, lakini tunafikiria kuipunguza zaidi au kuondoa kabisa kodi ili kuwezesha Watanzania wote wenye seti za televisheni kupata matangazo ya runinga,” alisema Makamba.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Profesa John Mkoma alisema Tanzania inajivunia kufanikiwa kutekeleza malengo ya kimataifa ya kuhamia mfumo wa dijitali kutoka analojia kulinganisha na nchi zingine za SADC.
Alisema matumizi ya king’amuzi imerahisisha gharama za matangazo ambapo hivi sasa mtu anaweza kurekodi kipindi na kukipeleka kwenye kituo cha Tv au redio kwa ajili ya kurushwa hewani.
Profesa Mkoma alisema matumizi ya dijitali pia yameboresha usikivu wa sauti na muonekano wa picha kwenye vituo vya televisheni nchini.
Tanzania ilianza kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa kuzima mitambo ya analojia kuanzia mwishoni mwa mwaka jana kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam mpango ulioendelea kwa mikoa mingine ya Tanzania.
Tayari baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki yameanza kufuata hatua hiyo ya Tanzania.

Tuesday, October 22, 2013

Wanafunzi Waliokosa mikopo vyuoni wahurumiwa...!!

WANAFUNZI 1,107 wa masomo ya kipaumbele waliokosa mkopo kutokana na fomu zao za maombi kuwa na dosari, wamehurumiwa na Serikali na sasa watapata mikopo waanze chuo.
Wanafunzi watakaonufaika ni wa ualimu wa hisabati (20), ualimu wa sayansi (164), wanafunzi wa sayansi na tiba (111), uhandisi –umwagiliaji (7), ualimu (617), sayansi ya kilimo (20), uhandisi (70) na sayansi (98).

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Serikali imeamua kutoa nafasi ya pili kwa wanafunzi hao kwa kutafuta fedha kutoka maeneo mengine tofauti na bajeti iliyokuwepo.
Kwa mujibu wa Mulugo, baada ya wanafunzi hao kushindwa kukidhi masharti kwa fomu zao kuwa na dosari, fedha za bajeti zilizokuwa zimepangwa kwa ajili yao, zilitolewa kwa wanafunzi wengine ambao hawakuwa wa kipaumbele.
“Ni kweli kosa limefanyika na Bodi (Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, HESLB)… pamoja na kuwa na haki kisheria kuhamisha fedha kwa wanafunzi wengine, walitakiwa kushauriana na Wizara kabla ya uamuzi huo ili kupata maoni ya nini kifanyike.
“Sasa tumefikia uamuzi wa kuwapa nafasi nyingine wanafunzi wenye masomo ya vipaumbele… wanatakiwa kurekebisha dosari zao wakishindwa kufanya hivyo wakati huu, hakutakuwa na huruma tena na fedha tutawapa wahitaji wengine wazingatie hili,” alisema na kuongeza kuwa majina ya wanufaika yatatangazwa na Bodi.
Mfuko wakung’utwa, mgawanyo
Akielezea namna watakavyopata fedha nje ya bajeti iliyopangwa, Mulugo alisema HESLB itatafuta Sh bilioni 2 kutoka kwenye makusanyo ya wadeni au fedha za matumizi mengine, na Wizara itatoa Sh bilioni 1.1 ili kufikisha Sh bilioni 3.1 zitakazotumiwa na wanafunzi hao.
Akifafanua mchaganuo huo, Mulugo alisema zaidi ya Sh bilioni 1.9 zitatumika kwa ajili ya chakula na malazi, Sh milioni 221.4 kwa ajili ya vitabu na viandikio, Sh milioni 686.34 kwa ajili ya mafunzo ya vitendo na Sh milioni 221.4 za mahitaji maalumu ya vitivo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu, alisema kutokana na bajeti iliyotengwa, wanafunzi 31,539 kati ya wanafunzi 31,647 sawa na asilimia 99.6, walitarajiwa kupatiwa mikopo.
Asilimia 83 ya wanafunzi hao kwa mujibu wa Bangu, wamedahiliwa katika kozi za kipaumbele na kati yao, asilimia 44 wamedahiliwa katika kozi ya ualimu zisizo za sayansi.
Aidha asilimia 29 wamedahiliwa katika kozi za kipaumbele za sayansi ya tiba, ualimu wa hisabati, ualimu wa sayansi, uhandisi wa mwagiliaji, uhandisi na sayansi za wanyama, wakati asilimia 17 ni wanafunzi wa kozi zingine zisizo za kipaumbele.
Bangu alisema katika mwaka wa masomo 2013/2014, Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB, iliidhinisha Sh bilioni 325 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo Sh bilioni 306 zilitoka serikalini na Sh bilioni 19 zilitokana na marejesho ya mikopo.
Lengo la bajeti hiyo ni kukopesha wanafunzi 94,023, wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.
Vyuo kukopwa
Akielezea wapi wanafunzi hao watapata fedha za kulipa ada ya chuo, Mulugo alisema;” Katibu (Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome) anakwenda kuandikia barua vyuo viwapokee wanafunzi hao na suala la ada liwe deni kwa Serikali. “Tutalipa deni hilo katika bajeti ijayo” alisema Mulugo.

Sunday, October 20, 2013

Ufoo Saro afunguka...!!

Ufoo Saro amehojiwa na Rai leo, na haya ndio aliyokuwa nayo ya kusema baada ya tukio la kupigwa Risasi..


MWANDISHI  wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, ameanza kufunguka kidogo kidogo na kueleza kwa kina jinsi tukio zima lilivyotokea. 

Akizungumza kwa sauti ndogo na taratibu na gazeti hili kando ya kitanda alicholazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mwanahabari huyo alieleza kushangazwa na ujasiri na nguvu za aina yake ambazo zilimwezesha kutambaa na kujiburuza hadi eneo la karibu ya barabara ili kuomba msaada wa kukimbizwa hospitali.

Ufoo ambaye alionyesha dhahiri kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazozingira tukio lake, alisema tayari alikuwa amewahakikishia polisi waliofika kumjulia hali hospitalini hapo kwamba alikuwa akisubiri afya yake iimarike kabla hajaeleza kwa kina kila anachokijua kuhusiana na tukio hilo.

“Alifika hapa kunijulia hali na kuangalia maendeleo yangu afande Msangi na nikasema nitakuwa tayari kueleza kila ninachokijua baada ya afya yangu kuimarika. Nasikitika kuna watu wanasema mambo wakifikia hatua ya kutaka kuonekana wananifahamu vizuri kuliko hata ninavyojifahamu mwenyewe,” alisema akionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kuhusu sakata lake.

Ufoo ambaye alifikishwa hospitalini hapo Jumapili ya wiki iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa risasi na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja alisema anamshukuru sana Mungu kwa uzima alionao sambamba na kuelezwa kupata faraja kubwa na kutiwa moyo na mwajiri wake, ndugu, jamaa na marafiki.    

Mwanahabari huyo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwake siku chache zilizopita, amelazwa katika chumba cha peke yake ambacho ingawa kina seti ya televisheni alisema alikuwa haruhusiwi kuiangalia kwa ushauri na maelekezo ya madaktari.

Huku akionekana wa chini ya uangalizi mwingine wa karibu na wa kudumu wa muuguzi ambaye muda wote wa mazungumzo haya alionekana kuwapo katika chumba hicho, Ufoo alisema alikuwa ana mapenzi makubwa kwa mzazi mwenzake huyo ambaye alipoteza maisha katika tukio hilo.

“Nilimpenda sana Antheri. Alikuwa kijana mtaratibu na mpole sana. Najua kile kilichotokea ni shetani tu na binafsi nilishasamehe alfajiri ile ile baada ya tukio lile,” alieleza Ufoo ambaye pia alimpoteza mama yake mzazi katika mkasa huo.
TUKIO ZIMA LILIVYOTOKEA
Ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya Antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.

Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, Ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea Sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (Ufoo) eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya kufika Kibamba na kwa sababu ambazo Ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.

“Hata sijui ni nini kilitokea. Wakati tukitoka nyumbani Antheri alianza kwa kuniambia kwamba alikuwa amepanga kujiua yeye na mtoto wetu,” alisema Ufoo kabla ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa na kuendelea na simulizi yake ya kusikitisha.

Akiwa na sura ya ujasiri, Ufoo anasema pamoja na kumwambia maneno hayo bado Mushi alimsisitiza kwamba waende kwa mama yake (Ufoo) baadae warudi kumchukua mtoto wao japo Ufoo hakusema walitaka kwenda wapi baada ya hapo.

Alisema walipofika nyumbani kwa mama yake walikwenda moja kwa moja sebuleni na wakiwa wamekaa kwenye makochi baada ya salamu za hapa na pale ghafla Mushi akasimama akamwambia mama yake Ufoo kwamba; “Mama nimeishafanya maamuzi”  

Kwa mujibu wa maelezo ya Ufoo, baada ya Mushi kutamka maneno hayo ghafla akaingiza mkono nyuma ya suruali  alikokuwa ameweka bastola  yake na kisha akaichomoa.

Katika maelezo yake Ufoo alisema baada ya kuichomoa bastola hiyo mama yake naye alisimama na kwenda kujaribu kumpokonya, kitendo hicho kilimfanya amiminiwe risasi mfululizo.

Alisema kuona hivyo aliamua kukimbia kuelekea jikoni ambapo Mushi alimuona na kuanza kumiminia risasi ambayo moja ilimpata eneo la mkono wa kulia ambayo ilitokezea mbele na kuchana titi la kulia.

Kwa mujibu wa Ufoo jeraha hilo halikumfanya akate tamaa ya kunusuru maisha yake kwani alijaribu kukimbia ingawa Antheri alifyatua risasi nyingine kadhaa ambazo zilimpata juu kidogo ya mgongo na kutokea tumboni ambazo zilisababisha aanguke chini 

Akiendelea kusimulia, anasema ingawa alikuwa akivuja damu nyingi, na huku akijiburuza ardhini, Ufoo alisema wakati akitambaa aligeuka nyuma na akamuona Antheri akijielekeza bastola eneo la kidevu na alipofyatua risasi alianguka chini.

“Nikiwa chini nilimuona Antheri akijipiga risasi kidevuni na akaanguka chini, sikujua kilichofuata baada ya hapo kwani niliendelea kujiburuza ili kuokoa maisha yangu,” alisema Ufoo  
ALIVYOJIOKOA 
“Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”. 

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema Ufoo. 

Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya Tumbi na akakubali.

“Yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.

“Wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini.

Alisema anakumbuka wakati walipofika eneo la Kibaha ilipo mizani ya kupima uzito wa magari makubwa walikuta barabara ikiwa imejaa magari na yeye alimuomba dereva huyo wa bodaboda kupita hata nje ya barabara eneo la nyasi ili kumwahisha hospitalini jambo ambalo kijana yule alilifanya.  

“Nilipofika eneo la mapokezi pale Tumbi nilimueleza muuguzi niliyemkuta kwamba nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi na nikamuomba asaidie kuokoa maisha yangu. Yule nesi alisita akitaka kwanza kupata kibali cha polisi (PF3) lakini nikaumuomba apigiwe simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Tumbi, Dk. Dattan ambaye tunafahamiana” 

“Baada ya muda mfupi Dk. Dattan alifika na nikamweleza yaliyonipata na mara moja nikaanza kuhudumiwa kwa kuniwekea dripu, na nikamsikia akiwaeleza wauguzi kwamba isingekuwa busara kwa hali niliyonayo kama wangeanza kuchukua picha za X-ray kwani hatua hizo zingeweza kusababisha kupoteza maisha,” alieleza akikumbuka yaliyojiri hapo Tumbi. 

Kwa mujibu wa Ufoo, akiwa bado ana fahamu alimsikia daktari aliyekuwa akimhudumia akiomba msaada wa gari la kubeba wagonjwa ili limchukue na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wito ambao ulijibiwa kwa maelezo kwamba lilikuwa halina mafuta.

Majibu hayo kwa mujibu wa Ufoo, yalisababisha daktari huyo aombe kuletewa gari la wagonjwa la wagonjwa maarufu (VIP) ambalo lililitwa na muda mfupi baadaye akapakizwa tayari kwa safari ya kukimbizwa Muhimbili. 

Alisema wakati akikimbizwa Muhimbili anakumbuka namna alivyokuwa akipatwa na maumivu makali wakati wote gari ile ya wagonjwa ilipokuwa ikipanda matuta ya barabarani na kuna nyakati alikuwa akihisi kupoteza pumzi na kuishiwa nguvu. 
KILICHOMUOKOA 
Akizungumzia kuhusu kile kilichonusuru maisha yake, mwanahabari huyo anasema, anaamini Mungu alisikia maombi yake na ya watu mbalimbali ambao walijitoa kumuombea na kumhudumia.

“Kwa muda wote tangu nilipopigwa risasi nilikuwa nikisali na kumuomba Mungu aniokoe na kunipa ujasiri. Niliomba sala zote ninazozijua. Namshukuru Mungu kwa kuniponya,” alieleza.

Akiendelea alieleza kushangazwa na ujasiri aliokuwa nao siku ile kwani hata baada ya kujiona akivuja damu kwa wingi alihisi kama vile mwili wake ulikuwa umekufa ganzi na akaendelea kujipa moyo na nguvu za kufika hospitalini kwa matibabu.

Source: Rai Nguvu ya hoja

Friday, October 18, 2013

Exclusive Video of what happened inside Westgate Mall

This footage obtained exclusively by CNN show the moment attackers entered the Westgate mall in Nairobi. 

Large part of the footage has been edited as is too horrific for broadcasting 

Friday, October 11, 2013

MAGAZETI YA LEO.. FRIDAY, OCTOBER 11, 2013

DSC 0059 cbb36
DSC 0060 33282DSC 0061 02d88
DSC 0062 0a52c
DSC 0063 15975
DSC 0064 e13e9
DSC 0065 ad282

DSC 0066 6c716
DSC 0067 bd738

DSC 0068 e95f5

DSC 0069 adbac

DSC 0070 abf2e

DSC 0071 7c543

DSC 0072 3b2d9

DSC 0073 bc248

DSC 0074 0e440

SPORTS: Rooney afunguka kuhusu Ferguson!!!

Manchester, England. Kitendo cha kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson kumhamisha nafasi anayocheza uwanjani Wayne Rooney kilitaka kusababisha nyota huyo kutaka kuihama klabu hiyo msimu uliopita, lakini uongozi wa klabu hiyo ulikataa kumuuza.
“Kila mtu katika klabu yetu anajua nafasi ninayotaka kucheza, kitendo cha kocha Ferguson kunichezesha nafasi tofauti kiliniudhi, kocha alikuwa akitaka nicheze nafasi ya kiungo, mimi sikutaka kucheza nafasi hiyo,”alisema Rooney.


Alisema “Ni kweli katika mechi nilizocheza nafasi ya kiungo nilicheza vizuri, lakini ni wazi nilikuwa sitaki kucheza nafasi hiyo, kwa hiyo nilimwambia kocha nataka kucheza nafasi ninayostahili kucheza ambayo ni nafasi ya ushambuliaji, lakini kocha akawa hataki.”
Rooney anasema,”Nafikiri jambo kama hilo kisaikolojia lazima litakuathiri, mimi liliniathiri katika baadhi ya mechi, najua msimu uliopita haukuwa mzuri, lakini sababu kubwa ni kwamba katika mechi nyingi kocha alikuwa hanipangi katika nafasi niliyokuwa nastahili kucheza.” Ingawa Rooney ameongelea sababu hizo zilizosababisha akose furaha katika klabu ya Manchester United msimu uliopita, anasema hakuwa na tatizo na klabu hiyo katika kipindi cha usajili msimu huu.
“Kwa kweli katika kipindi chote cha usajili msimu huu  nilikuwa nimetulia na kufurahia maisha, mke na mimi tulikuwa tumepata mtoto mwingine,” alisema Rooney.
Alisema,”Msimu huu nimefanya kazi kwa bidii katika klabu ya Mancheter United, niliumia kwa sababu ya kufanya kazi kwa bidii, nina mtazamo mzuri na nataka kuwathibitishia watu kwamba mimi ni mchezaji wa kiwango cha juu.”
Wakati wa kipindi cha usajili msimu huu, klabu ya Manchester United ilikataa mara mbili ofa ya Chelsea kutaka kumsajili Rooney, ambapo mchezaji huyo katika kipindi chote hicho alikaa kimya katika kulizungumzia suala hilo.
“Nilikaa kimya na kuacha kulizungumzia suala hilo kwa sababu nilikuwa nikijua klabu itatoa msimamo wake na ndivyo ilivyofanya kwani ilikataa ofa za klabu zilizokuwa zikinitaka,”alisema Rooney.
Alisema,”mimi nilizungumza na viongozi wa klabu na kuwaachia suala hilo, sikulizungumzia suala hilo kwenye vyombo vya habari kwa sababu nilitaka kutulia na kuweka mtazamo wangu katika soka.”