Blogger Widgets

Thursday, November 13, 2014

BREAKING NEWS: Msanii wa HipHop Geez Mabovu afariki Dunia..

Geez Mabovu
Geez Mabovu ni ambae hajavaa shati.
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2

Friday, November 7, 2014

MPYA HII KUTOKA WHATSAPP,, WAONGO SASA BAASI..

whatsapp-doble-checkNakumbuka moja ya taarifa kubwa zilizowahi kuchukua headlines mwezi Februari 2014 ilikuwa ni stori ya kuuzwa kwa mtandao wa Whatsapp kwa mmiliki wa Facebook, leo kuna taarifa nyingine mpya kuhusiana na watumiaji wa mtandao wa Watsapp.
Haya ni mambo manne mapya ambayo huenda hujayasikia kuhusu WhatsApp;-
1. Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
2. Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
3. Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
4. Ukibonyeza ujumbe uliotuma utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
whatsapp
Kuanzia jana huduma hiyo itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Ukibonyeza ujumbe wenyewe itakuonyesha muda ambao uliyemtumia ujumbe huo kausoma.
Tazama video hii uone mabadiliko hayo.

BRAND NEW: HII NDIO TRACK YA GOSBY INAYOITWA "WEMA SEPETU" ILIYO MAKE HEADLINES..

Gosby
Kila alieona jina la wimbo ‘Wema Sepetu’ amekua na hamu ya kujua moja kwa moja nini kimeimbwa ndani ya hii single ya mkali Gosby ambayo single zake zilizotangulia kama ile ya ‘Monifere’ ft. Vanessa Mdee zimempa nafasi ya kupokewa zaidi na Wabongo.
Ukitaka kuisikiliza na kudownload hii mpya ya ‘Wema Sepetu’ unaweza kubonyeza hapa

DOWNLOAD 

Saturday, November 1, 2014

HAYA NDIYO ALIYOSEMA CHID BENZ KUHUSIANA NA YE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AIRPORT..

Screen Shot 2014-11-01 at 3.14.15 AMImekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.
Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
Screen Shot 2014-11-01 at 3.14.00 AMKuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>> ‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake… tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji, tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’
Screen Shot 2014-11-01 at 3.39.11 AMKuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’
Screen Shot 2014-11-01 at 3.44.09 AM‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe’
‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.