Blogger Widgets

Friday, February 20, 2015

VIDEO: Cheki "Behind the Scenes" Ya Video mpya ya Diamond na Linex

Hizi ni clip za utengenezwaji wa Video mpya ya Diamond na Linex.. Behind the scenes.. Jionee hapa.. Video inatengenezwa na Adam Juma..

 

TAARIFA YA MSIBA WA MSANII WA BONGO FLEVA, MEZ B

Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
MEZ-B2
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarifu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Noorah, Dark Master na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.

BRAND NEW AUDIO: Jux - Nikuite Nani. Sikiliza na Download hapa..

Hii Ndio Track mpya kutoka kwa Jux,, Wimbo unaitwa Nikuite Nani, Umetengenezwa AM Records..