ALJERRY'12
Wednesday, February 10, 2016
New Music: Listen, Download and Support this Upcoming Artist..
Kwa support tuliyopata toka kwa Viewers wa blogyetu toka kuanzishwa kwake ndiyo iliyotufikisha hapatulipo,, And now its our turn to pay back. This is us supporting Underground Music, trying to take Tanzanian Music to that New Level,, KWa Moyo Wa Dhati tunakuomba Sikiliza na Download Nyimbo hii toka kwa Msanii Mchanga Bless, Then Tupe maoni yako kusaidia kuendeleza mziki wa kizazi kipya Tanzania.
Tumerudi Tena na Hizi za Mkude Simba, Sikiliza na Download Hapa..
Baada ya kimya Kirefu, Sasa tunarudi tena na hizi kutoka Kwa Mkude Simba,, Bofya hapa Kusikiliza na ku Download...
Wednesday, October 28, 2015
HAYA NDIO MAAMUZI MAPYA JUU YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR..!!
MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR YAMEFUTWA, Madai ni kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na Haki
Sababu nyingine iliyochangia kufutwa kwa matokeo hayo ni pamoja na ikiukwaji wa sheria ikiwemo mgombea Maalim Seif kujitangaza kwenye matokeo kuwa mshindi.
Via AzamTV
Thursday, September 3, 2015
SIRI, HOTUBA YA DK. SLAA..
Hotuba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, imepondwa vikali na wasomi mbalimbali wasiofungamana na upande wowote kisiasa.
Juzi Dk. Slaa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kufuatia kujiweka kando kujishughulisha na Chadema kutokana na na chama hicho kumpokea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kumpitisha kugombea nafasi ya urais akiviwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ajitokeza hadharani na kutoa msimamo wake wa kustaafu siasa, huku akimtuhumu mgombea huyo kuwa alihusika moja kwa moja na sakata la Richmond, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kwa jamii.
Mkufunzi Msaidizi kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Godlisten Malisa, alipotakiwa na Nipashe kutoa maoni yake, alisema pamoja na kukubaliana na hotuba ya Dk. Slaa, lakini haikutolewa katika muda muafaka.
“Dk. Slaa ni kiongozi anayeheshimika kutokana na mchango wake mkubwa wa kuuimarisha upinzani na hasa Chadema, lakini alichokisema na hasa dhidi ya Lowassa kilipaswa kusemwa wakati wa mchakato wa kumpokea Chadema ama kabla ya kuingia kwenye kipindi cha kampeni,” alisema.
Malisa alisema, alipaswa kusema kabla, ili kuwasaidia watu ambao tayari wameshaamua kuwa na Lowassa na pengine kumpigia kura kutokana na ushawishi wa kampeni zinazoendelea, na hivyo hotuba yake hiyo kutokuwa ya msaada sana kwa wakati huu.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Alexander Makulilo, alisema uamuzi alioufanya Dk. Slaa ni haki ya kidemokrasia ya mtu kama sheria za nchi zinavyoeleza.
“Alichokifanya ni haki ya kidemokrasia kwa kuwa katiba ya nchi imeeleza mtu halazimishwi kuwa chama fulani bali ni utashi wake,” alisema Dk. Makulilo.
Aidha, alisema kitendo hicho hakina haja ya kupingwa kwa kuwa watu wengi ni wafuasi na siyo wanachama.
Naye Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Idara ya Mawasiliano, Danford Kitwana, alisema amesikitishwa na kitendo cha Dk. Slaa ambaye anaamimika kuwa na dhamira ya kulikomboa taifa na kuliletea mabadiliko baada ya kusema Chadema kimaadili kibaya kuliko chama tawala.
Kitwana alisema hana tatizo na mtazamo alioutoa Dk. Slaa, bali mashaka yanakuja kutokana na hotuba yake kuonyesha mafisadi wapo Chadema wakati inaaminika CCM ndicho chenye idadi kubwa ya mafisadi.
Profesa wa uchumi, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Prosper Ngowi, amesema kujiuzulu kwa Dk. Slaa kumetokana na upeo na mtazamo alionao kiongozi huyo katika kutazama mambo.
Prof. Ngowi alisema uamuzi wa kujiweka pembeni na siasa ya vyama au kushiriki ni hiari ya mtu hailazimishwi.
Saturday, July 11, 2015
PICHA ZA KINACHOENDELEA DODOMA, MAKAO MAKUU YA CCM MUDA HUU..!!

Kikao cha Halmashauri Kuu kimeendelea sasa hivi kwa zaidi ya saa nne hapa Makao Makuu ya CCM Dodoma, viko vitu vingi vinaendelea nje ya Ukumbi… wapo wanaoimba na kushangilia, wengine wapo wakiendelea kusubiri kile kitakachotangazwa baada ya Halmashauri Kuu kumaliza Kikao.
Watu ni wengi sana nje ya Ukumbi, nimebahatika kukutana na wenyeji wa Mji wa Dodoma na watu ambao wanafanya shughuli zao kwenye Majengo yanayozunguka Makao Makuu hayo, wanasema haikuwahi kutokea mtaa huu ukawa busy watu wakawa wengi kiasi hiki.
KUTOKA DODOMA,, HAWA NDIO WAGOMBEA WATANO WALIOTAJWA NA CCM..!!
July 10 2015 inaripotiwa taarifa nyingine kutoka Dodoma Tanzania… Watu wengi wamekaa tayari kujua nini ambacho kitaamriwa Dodoma kuhusu Mgombea Urais ambae anateuliwa na CCM kugombea Urais wa Tanzania 2015.
Majina yalikuwa mengi zaidi ya 38, hii ndio list ambayo imetangazwa kuingia Top Five kupitia ukurasa wa Twitter wa CCM @ccm_tanzania
Sunday, June 14, 2015
NA HII NDIYO LIST YA WASHINDI WOTE WA TUZO ZA KTMA..
Bendi Bora ya Mwaka - FM Academia
Wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa - MwanaFA ft. Ali Kiba - Kiboko Yangu
Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia - Barakah Da Prince
Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Tanzania - Waite - Mrisho Mpoto
Wimbo bora wa Zouk/Rhumba - Ntampata Wapi - Diamond Platnumz
Wimbo bora wa Afro-Pop - Mwana - Ali Kiba
Video ya bora ya muziki ya Mwaka - Mdogo Mdogo - Diamond Platnumz
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka bendi - Amoroso
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka Bongo Flava - Nahreel
Mtunzi bora wa mwaka Hip Hop - JohMakini
Mtunzi bora wa mwaka bendi - Jose Mara
Mtunzi bora wa mwaka Bongo Flava - Ali Kiba
Mtunzi Bora wa mwaka Taarab - Mzee Yusuf
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki - Sura Yako - SautiSol
Msanii Bora wa Hip Hop - JohMakini
Rapper bora wa mwaka bendi - Ferguson
Wimbo bora wa reggae/dancehall - Maua Sama
Wimbo bora wa Hip Hop - Kipi Sijasikia - Prof Jay ft. Diamond Platnumz
Wimbo Bora wa R&B - Sisikii - Jux
Wimbo Bora wa Kiswahili Bendi - Wale Wale - FM Academia
Wimbo Bora wa Mwaka - Mwana - Ali Kiba
Wimbo bora wa Taarab - Mapenzi Hayana Dhamana - Isha Mashauzi
Muimbaji Bora wa Kiume Bendi - Jose Mara
Mwimbaji Bora wa kike Taarab - Isha Mashauzi
Mwimbaji Bora wa Kiume Taarab - Mzee Yusuf
Muimbaji Bora wa Kike Bongo Flava - Vanessa Mdee
Muimbaji Bora wa Kiume Bongo Flava - Ali Kiba
Mtumbuizaji bora wa muziki wa mwaka wa kike - Vanessa Mdee
Mtumbuizaji bora wa muziki wa mwaka wa kiume - Ali Kiba
Subscribe to:
Posts (Atom)