Blogger Widgets

Monday, June 17, 2013

KAULI YA RAIS KUTOKANA NA MLIPUKO ULIOTOKEA ARUSHA!!

MLIPUKO wa bomu uliotokea Arusha na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 70 limezua utata kutokana na hisia tofauti za viongozi mbalimbali nchini waliozungumzia suala hilo, huku Rais Jakaya Kikwete akisema haamini kama Watanzania sasa wamefikia hatua ya kuanza kuhasimiana kwa misingi ya kisiasa.
Hii ni mara ya pili kwa Jiji la Arusha kushambuliwa kwa bomu baada  ya lile lililorushwa kwenye Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi kwenye Parokia ya Olasiti wakati wa sherehe ya uzinduzi wake Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu na kujeruhi 64. Wakati Rais Kikwete akisema hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wamesema tukio hilo ni la kisiasa na lilipangwa.
Kufuatia tukio hilo, uchaguzi wa  kata nne za Arusha mjini umeahirishwa hadi Juni 30.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana imeeleza kuwa Rais Kikwete ambaye yuko nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa nchi zilivyoendelea kiviwanda(G8), alisema haamini kama Watanzania ama wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kudiriki kufanya matukio ambayo yanahatarisha usalama wa watu.
“Mimi   siamini   kuwa  Watanzania au wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kufanyiana matendo ya unyama wa aina hii. Naamini kuwa hiki ni kitendo cha mtu ama watu wasioitakia mema nchi yetu, watu ambao wanatafuta kila sababu ya kupandikiza chuki miongoni mwa raia ama makundi ya raia, ili nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa.”