Blogger Widgets

Friday, June 14, 2013

Woman, Mistaken for Dead, dies for real of Heart attack After waking up at own funeral!!!!

Woman, Mistaken for Dead, dies for real of Heart attack After waking up at own funeral!!!!




Mwanamke mmoja raia wa Urusi, alifariki ghafla kwa mshtuko wa Moyo baada ya kuamka na kujoikuta katika msiba wake mwenyewe. Fagilyu Mukhametzyanov, 49, alithibitishwa kimakosa na Madaktari kuwa amekufa, angali bado alikuwa mzima, hivyo taratibu za maziko zikafanywa tayari kwa mwanamke huyo kuzikwa.

Kwa hali isiyo ya kawaida, baadae mama huyu alizinduka na kujikuta katika jeneza akiwa amezungukwa na ndugu zake wakiomboleza, ndipo alipoanza kupiga mayowe baada ya kugundua alikuwa anakaribia kuzikwa mzima.
Mukhametzyanov, mkazi wa Kazan, Russia, alipatwa tena na mshtuko baada ya tukio hilo na kukimbizwa tena hospitali na kuthibitishwa kuwa amekufa tena kwa mara ya pili, lakini sasa ilikuwa ni kweli!!!