Blogger Widgets

Tuesday, July 2, 2013

Mhe. Rais Obama atembelea Mitambo ya Symbion na kuzindua mpango wa maendeleo ya nishati Afrika

Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama akizindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani  (Power Africa Initiative) wakati alipotembelea Mitambo ya Kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo Jijini Dar es Salaam katika siku yake ya pili ya ziara ya kitaifa hapa nchini.
Wageni mbalimbali wakiwemo Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini wakimsikiliza Mhe. Rais Obama
Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakimsikiliza mmoja wa Wataalam aliyebuni kifaa mfano wa mpira ambapo kinapojaa upepo kwa kupigwa huweza kusababisha nishati ya umeme ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali kama kuchaji simu na kuwasha taa.

Mheshimiwa akionesha umahiri wake kwenye ball control kwa kutumia kiffa hicho chenye mfano wa mpira wa miguu!!
Mhe. Rais Obama na Mhe.Kikwete wakijaribu kupigiana kifaa hicho mfano wa mpira.




Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakiangalia kifaa hicho kikiunganishwa kwenye moja ya taa kabla ya kuwashwa.