Blogger Widgets

Wednesday, August 7, 2013

Mfanyabiashara Maarufu wa Madini Auwawa kwa kupigwa Risasi Arusha!!

ARUSHA: Mfanyabiashara maarufu wa madini Mererani na Mmiliki wa SG RESORT ya Arusha, Bw. Erasto Msuya ameuwawa leo majira ya alasiri wakati alipokuwa akitokea Mererani kuelekea Moshi. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana mara baada ya tukio hilo zinasema kuwa mfanyabiashara huyo alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mara baada ya majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya barabara ya kia. inasemekana wauaji wamekimbia na briefcase yake.