Blogger Widgets

Sunday, August 25, 2013

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Viongozi wengine wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Iringa!

Mwenyekiti Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa la kuzidisha muda wa mkutano.

Polisi wanasema mkutano ulimalizika saa 12.30 badala ya saa 12.00

Source: Jamii Forums 

Swali lwa msingi kwa Polisi, sheria gani wanayotumia katika suala hili. Au ni ule mwendelezo wa kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa.

Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Jeshi la Polisi, zote hazizungumzii muda specific wa kufunga mkutano, bali sun set. Kwa sababu sun set inategemea geographical location. Maeneo kama Kigoma saa 1 jioni, jua linawaka kama vile saa 12.

Ni Sheria ya Uchaguzi pekee, ndiyo inazungumzia muda maalum ambao ni 12.30. Na ni kwa sababu ya mazingira ya equality kwa ajili ya wagombea wote kufanya kampeni ndani ya muda mmoja.