Blogger Widgets

Thursday, September 26, 2013

Ufugaji wa aina hii Handeni haukubaliki..!!

Leo naomba tuachane na habari zetu za historia na utalii. Ninataka kuzungumzia uharibifu wa mazingira kama nilivyoshuhudia huko Handeni mkoani Tanga katika Kijiji cha Nyasa, vitongoji vya Kariakoo na Ubungo.
Ng’ombe wakiwa Hifadhi ya Msitu wa Nyasa, kitongoji cha Ubungo. Picha ya Maktaba. 
Maeneo hayo yanaendesha shughuli za ufugaji, kilimo na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Awali eneo hilo lilikuwa ni hifadhi ya msitu, likaondolewa katika hifadhi ya msitu, lakini kwa kweli uchimbaji wenyewe na ufugaji unaharibu mazingira kwa kasi ambayo kama haitadhibitiwa mambo hayatakuwa mazuri katika siku za usoni.
Eneo hilo limevamiwa na wafugaji ambao wanalisha mifugo yao bila kujali kwamba wanaharibu ardhi, uoto wa asili na kusababisha  jangwa. Wanyama hao wanalishwa hovyo, unapowaona utadhani umekutana na makundi ya nyati katika mbuga za wanyama.
Nilishawahi kuandika wakati fulani kuwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji unatakona na kuendekeza aina ya ufugaji ambao hauzingatii maarifa na teknolojia ya kisasa.
Tulipowaona ng’ombe hao moja ya wazo ni kuwa unaweza kuwadhibiti wasiingie kwenye mashamba ya wakulima kama wanalishwa kwa makundi makubwa ya ng’ombe 300  au zaidi.
Serikali inapaswa kuachana na maneno matupu kuhusu kuingiza maarifa ya kisasa katika shughuli za kilimo na ufugaji. Handeni katika msimu uliopita kulikuwa na tatizo la njaa na moja ya sababu ni kukosekana kwa mvua za kutosha.
Ufugaji wa kuharibu misitu na mazingira ya maji unaoendeshwa huko hauwezi kuwa rafiki ila kuongeza tatizo lingine ambalo limekuwapo huko kwa muda mrefu.
  Inashangaza sana kwa Serikali kuwa wawekezaji wakubwa wanapotaka kufanya shughuli za uchimbaji, Baraza la Taifa la Mazingira (Nemc) linawasimamia, lakini Nemc hiyo hiyo inanyamaza kimya pale wahusika wanapoharibu mazingira hasa  wachimbaji wadogo.
Source: Mwananchi