Blogger Widgets

Tuesday, June 17, 2014

Hii Kali,, Cheki mwimbaji huyu anavyoipenda sauti yake hadi kuchukua uamuzi huu..!!!

bg
Mwimbaji Alama Kante, amelazimika kuimba huku akifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye koo lake ili madaktari wasiharibu sauti yake.
Mwimbaji huyo kutoka Guinea mwenye makazi yake nchini Ufaransa alipatiwa dawa za kumfanya asisikie maumivu wala uchungu wakati wote wa zoezi la upasuaji.
Kante alikuwa akiogopa kupoteza sauti yake lakini daktari wake alipendekeza afanyiwe upasuaji huku anaimba.
Kante ambaye kwa sasa amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na wakati alipoamka na kuzungumza tena madaktari na wauguzi walifurahi kwakuwa wametimiza lengo lao..