Blogger Widgets

Sunday, June 29, 2014

Updates za kinachoendelea katika Tuzo za BET,, na Mshindi wa Tuzo ya Best African Act..!!

Habari mbaya kwa watanzania na wapenzi wote wa Bongo fleva. Msanii Davido toka Nigeria azidi kumpelekesha Diamond. Tuzo pekee aliyokuwa akiwania Diamond Platnumz imenyakuliwa na Davido. Diamond aliyekuwa Nominated katika Category ya Best African Act katika Tuzo za BET, amejikuta akishindwa tena mbele ya Mpinzani wake mkubwa Davido kama ilivyokuwa katika Tuzo za MTV, ambapo davido alishinda zidi ya Diamond katika kipengele cha Best Male Artist. Katika ukurasa wake wa Istagram, Davido alipost picha hii hapa chini..

Picha hii ilikuwa na caption inayosema "Thanks to all my fans!! WE WON Best African Act 2014!! so happy! Time to party!" 
Ujumbe huu unaonesha dhahiri Davido ndio mshindi wa tuzo hiyo..

Ukurasa huu unapenda kutoa pongezi Kwa Diamond Platnumz kwa kuiwakilisha vyema Tanzania, na kwa Hatua kubwa aliyofikia.. Usikate tamaa, huu ni mwanzo tu..